Licha yamipaka hiyo kufungwa, bidhaa bado zitaruhusiwa kuingia Kenya kutoka Tanzania na Somalia. Siku moja baada ya Kenya kufunga mpaka wake na Tanzania kwa siku 30 kuzuia ueneaji wa maambuziki ya Covid-19, Rais Magufuli amesema Tanzania haitafunga mipaka yake kwa sababu kwa kufanya hivyo itaathiri nchi jirani na biashara za Tanzania.
Mshukiwa wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda, Felicien Kabuga, ambaye anashutumiwa kuwa mmoja wafadhili wakuu katika mauaji ya kiasi cha watu laki nane, alikamatwa Jumamosi karibu na mji mkuu wa Ufansa, Paris, baada ya kujificha kwa miaka 26, ilisema wizara ya sheria ya Ufaransa.
Burundi inafanya uchaguzi wake mkuu wiki hii kuamua nani atachukua nafasi ya Rais wa sasa Pierre Nkurunziza anayemaliza muda wake na kisha kustaafu baada ya miaka 15 ya uongozi. Kampeni zimekuwa na machafuko na vurugu, huku serikali ikishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika jitihada zake za kuendelea kushikilia madaraka.