Wataalam nyumbani na ng'ambo, wametueleza kuwa chanjo zetu ni salama na fanisi. Ila, hadhithi nyingi za uongo kuhusu chanjo, bado zinasambazwa bila kuthibitishwa. Na hiyo inatuleta katika uongo wa mwisho ambao ni kwamba, chanjo hiyo ita umiza uwezo wako wakupata mimba katika siku za usoni.
Hakuna ushahidi kuwa chanjo yoyote ya coronavirus inayo tumiwa au, inayo undwa ita athiri uwezo wako wakuzaa au kuzalisha. Pengine kauli hiyo inachimbuko kutoka dhana kuwa, nchi nyingi zimependekeza wanawake, wasichanjwe wakati ni wajawazito ila, ni kwasababu chanjo hizo bado hazija pimwa kwa wanawake wajawazito.
Hiyo si ajabu, majaribio ya chanjo nyingi katika historia, hayaja wajumuisha wanawake wajawazito. Profesa Collignon amesema data kuhusu maisha baada yakuchanjwa kwa upande wauwezo wakuzaa au kuzalisha, itapatikana katika miezi na miaka ijayo. Ila, hatarajii matokoe yoyote yakushangaza