Je wahamiaji wanapokea taarifa gani kuhusu hali itakavyo kuwa, watakapo anza karantini ya wiki mbili nchini kabla waanze safari yao kuja nchini Australia?
Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na John, ambaye siku chache zilizo pita alimaliza karantini yake hotelini, na punde baadae akajipata chini ya vizuizi vilivyo dumu kwa muda wa siku tatu mjini Brisbane, baada ya kisa cha COVID-19 kutambuliwa mjini humo.