Makala haya ya mwongozo wa makazi, ni utangulizi kwa baadhi ya kanuni mhimu ambazo zinaweza shawishi tabia yetu, nakuheshimu maarifa na hadhi yakipekee yawa Australia wakwanza.
Itifaki za kitamaduni asilia zinatokana na kanuni za kimaadili zinazo unda mahusiano yetu yakikazi nakibinafsi nawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait.
Ni mhimu kutunza mahusiano haya kwasababu, wao ndiwo wa Australia wa kwanza. Wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, wana ujuzi wa ndani wa ardhi, na wanaweza tufunza mengi kuhusu jinsi yakujali mazingira yetu.