Mradi wa Global Talent Independent Visa, ni mradi wa viza ambayo imetengwa kwa watu wenye maarifa na ujuzi zaidi kote duniani, na nimoja ya viza inayotafutwa sana kwa makazi yakudumu nchini.
Kuanzia julai mosi 2020 hadi tarehe 8 januaria, idara ya maswala ya nyumbani ilipokea jumla ya nia zamaombi elfu saba mianne na sitini na saba, kwa mradi huo wa Global Talent Initiative Program.Katika wakati huo, raia wa Iran walipokea mialiko mingi zaidi ambayo ilikuwa ni 277, wakifuatwa na raia wa India ambao walikuwa (174), raia wa Bangladesh walikuwa(166), raia wa China walikuwa (133) na raia wa Uingereza walikuwa (103).
Kwa taarifa zaidi kwa jinsi unaweza omba viza chini ya mradi wa Global Talent Independent Program, tembelea tovuti ya idara yamambo ya ndani. Anwani yao ni: www.homeaffairs.gov.au/