Maelfu ya wakaaji wa NSW walio kuwa wame pata chanjo zote mbili za Uviko-19 walitazamia Jumatatu 11 Oktoba 2021, ambayo ilikuwa imebatizwa jina la "siku ya uhuru" kwa hamu sana. Hiyo ni siku ambayo wangeweza kutana namarafiki na jamaa wao tena pamoja nakupata huduma zote walizo kosa kwa zaidi ya siku 100.
Bw Jean D'amour ni mmoja wa wakaaji wa Sydney, ambao walikuwa wakisubiri siku hiyo ya ''uhuru'' kwa hamu, alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya SBS masaa machache baada ya watu walio kuwa wame pata chanjo zote mbili kuanza kujumuika katika jamii.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.