Hata hivyo, fursa hizo zakujumuika tena kwa walio pata chanjo kamili zimekuja na changamoto kadhaa hususan kwa baadhi ya wafanyakazi. Hoja ambayo imeibuka nikama wata endelea kufanyia kazi nyumbani, au itawabidi warejee maofisini tena baada ya muda mrefu wakufanyia kazi nyumbani.
Claude ni mmoja wa wafanyakazi wanao toa huduma katika shirika la IMS mjini Wollongong, shirika hilo huwahudumia wahamiaji na wakimbizi ndani ya jamii. Kwa muda mrefu Bw Claude na wafanyakazi wenza wamekuwa wakitolea huduma zao mtandaoni kuambatana na mwongozo wa mamlaka, ila sasa baada ya mwongozo kubadilika kwa walio pata chanjo kamili, Bw Claude na wafanyakazi wenza wamejipata katika njia panda kwa upande wa utoaji wa huduma zao nyumbani au ofisini. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Claude alifunguka kuhusu kitendawili hicho.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.