Je tiba ya coronavirus inapatikana ndani ya biblia?

Mwanamke asoma Biblia

Mwanamke asoma Biblia Source: pixelheadphoto

Waumini duniani kote huadhimisha pasaka kwaku jumuika kanisani na sehemu zingine maalum.


Ila mwaka huu virusi vya corona vimewalazimisha waumini na wachungaji, kutafuta mbinu mbadala zakushiriki katika maadhimisho ya pasaka.

Je wachungaji wanaunga mkono hatua zakukabiliana na coronavirus za watu kujitenga kijamii, kwa gharama yakutojumuika makanisani? Na je wachungaji wanakabilianaje na utabiri potovu, ambao baadhi ya waumini wanachangia katika mitandao yakijamii mojawapo ikiwa kwamba, ukipata nywele ndani ya biblia, na ukiiweka ndani ya chombo chenye maji nakunywa maji hayo utapata kinga ya maambukizi ya coronavirus.

Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na mchungaji David kutoka kanisa la Sing Hosana ambalo liko mjini Sydney, Australia. Mchungaji David alifunguka kuhusu jinsi yeye na wachungaji wenza, wanakabili changamoto zakuwahudumia waumini wakati wa janga hili la coronavirus.

 


Share