Je! Raia wana haki yakupewa taarifa kuhusu, hali ya afya ya viongozi wao?

Rais Kenyatta atoa hotuba

Rais Kenyatta ahotubia taifa kuhusu vizuizi vya covid-19 Source: State House Kenya

Viongozi kadhaa katika chama tawala nchini Tanzania, wakiongozwa na waziri mkuu wamekana madai yanayo endelea kusambaa kuwa, Rais Magufuli anapokea matibabu ya coronavirus nje ya nchi.


Madai hayo yamesambaa kwa kasi katika mitandao yakijamii ambako, baadhi ya watu wanadai Rais Magufuli yuko nchini Kenya akipokea matibabu ya Coronavirus, wakati wengine wanadai ame pelekwa nchini India kwa matibabu ya ziada.

Nako nchini Kenya, Rais Kenyatta ametangaza kuwa serikali yake inaongeza kipindi cha katazo la raia wake kutoka nje kati ya saa nne usiku, na saa kumi alfajiri kwa muda wa miezi mingine miwili. Wanasiasa nchini Kenya wamekuwa wakihudhuria mikutano mikubwa ya kisiasa kila wiki na wanaohudhuria wanaonekana kutofuata maagizo ya kujikinga. Wanaoandaa mikutano hawavai barakoa na mara nyingi wanaonekana kusalimiana na kupiga pambaja. Mikutano hii inatajwa kuwa chanzo cha kuambukizana kwa wingi.

Mmoja wa kaka pacha ambao walikuwa wanamuziki maarufu nchini Kenya Christian Longomba amefariki dunia. Kifo cha Christian kilitangazwa jana usiku na pacha mwenzake Lovy Longomba, ambao kwa pamoja walikuwa wanamuziki wapendwa wakati wao miaka ya 2000 maarufu kama 'Longombas'. Kaka yake Lovy Longomba alithibitisha kifo chake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram. Christian amekuwa mgonjwa tangu mwaka 2015 alipopatikana na uvimbe wa ubongo na kufanyiwa upasuaji nchini Marekani.


Share