Tangazo hilo limejiri baada ya serikali kuzingatia kuendelea kupungua kwa visa vya coronavirus jimboni.
Hili ni tangazo jipya kutoka kwa kiongozi wa jimbo kuhusu, jinsi watakavyo warejesha wanafunzi shuleni, hatua ambayo inatofautiana nchini kote. Ila hatua hiyo inasababisha hali yakuchanganikiwa miongoni mwa wazazi na walimu, ambao wanataka mwelekeo wa umoja.
Viongozi wote wamajimbo nchini wamekiri kuwa mipango yao, inaweza badilika wakati wowote.
Na unaweza pata taarifa mpya kuhusu janga la Coronavirus kwenye tovuti hii: sbs.com.au/Coronavirus.