Kukabiliana na baadhi ya dhana hizo potovu, viongozi wa jamii yawatanzania wanao ishi Victoria, wali waalika wataalam wa afya katika mkutano maalum, ambako walitoa taarifa kuhusu Uviko-19, chanjo husika pamoja nakujibu maswali ya wanajumuiya.
Masaa machache baada ya mkutano huo, kiongozi wa jamii hiyo Habib Chanzi, alieleza idyaa ya Kiswahili ya SBS, jinsi mkutano na taarifa iliyo tolewa na wataalam hao wa afya ilivyo pokewa na wanajumuiya walio shiriki.