Janga la COVID-19 lasababisha kufutwa kwa matukio na uharibifu katika soko za hisa

Dharura ya Coronavirus yasababisha mitaa ya Rome kuwa mitupu

Dharura ya Coronavirus yasababisha mitaa ya Rome kuwa mitupu Source: AAP

Duniani kote, janga la COVID-19 coronavirus limedai maisha mengi zaidi, limesababisha uharibifu mkubwa katika soko za hisa, biashara kadhaa zimefungwa pamoja na matukio mengi kufutwa.


Zaidi ya watu laki moja elfu ishirini na saba, katika zaidi ya nchi 110 wame ambukizwa virusi hivyo tayari.

Visa vingi vya maambukizi hayo viko katika nchi nne, China na Korea Kusini ambako visa vipya vinapungua na Iran na Italy ambako visa hivyo havipungui. Usambaaji huo umepungua kasi sana nchini China, kiasi kwamba serikali ya nchi hiyo imetuma kikosi cha maafisa wa afya nchini Italy, pamoja nakutuma msaada wa ziada nchini Iran na katika nchi zingine ambako msaada huo unahitajika.

Zaidi ya idadi ya watu elfu nne miasaba wamefariki tayari duniani kote kupitia virusi hivi vya covid 19 coronavirus.


Share