Wakazi kutoka mazingira ya uhamiaji katika miji pacha ya Albury na Wodonga, ambayo imegawanywa na mpaka wameripoti uwepo wa hali yakuchanganikiwa, pamoja nakuchelewa kupokea taarifa kwa muda wa hadi masaa 36.
Wakati huo huo serikali ya New South Wales imedokeza uwezekano wakuweka vizuizi vikali zaidi, kwa miji ambayo iko katika eneo la mpaka wake na Victoria.
Hatakama kiongozi wa New South Wales Gladys Berejiklian amesema, seriklai yake itasubiri kutekeleza hatua hiyo kwa sasa, amesema hali ya "tahadhari inaendelea kuwa juu".