Hatua za polisi kuimarishwa, baada yauvunjaji wa masharti ya karantini

Wasafiri wanao vaa barakoa wawasili katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Sydney, Australia

Wasafiri wanao vaa barakoa wawasili katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Sydney, Australia Source: AAP

Ukaguzi uliofanywa na shirika kubwa la huduma ya makazi ya wahamiaji, umepata kuwa zaidi ya takriban biashara ndogo 300, zilizo anzishwa na wakimbizi mjini Melbourne na Sydney, zime endeleza oparesheni zao wakati wa janga.


Ripoti hiyo imejiri wakati serikali ya Victoria imetangaza, kuregezwa kwa ziada kwa vizuizi, kwa matumizi ya barakoa pamoja navikomo kwa mikusanyiko katika mazingira mbali mbali.

Kuberesha zaidi namna yakutambua coronavirus katika viwanja vya ndege, mbwa wakunusa wanafunzwa kuweza kutambua virusi hivyo kabla matokeo chanya vya vipimo hayaja tokea. Mbwa hao wanafunzwa kutambua harufu fulani katika jasho, lengo likiwa kuwatumia mbwa hao pamoja na vipimo vya P-C-R kwa wasafiri wakimataifa kuanzia mapema mwakani.

Susan Hazel ni mtafiti kutoka chuo cha Adelaide, amesema mbwa hao wakunusa wakiwa na mafanikio, wanaweza kuwa fanisi kutambua virusi hivyo dalili zikiwa bado hazija tambuliwa. Na unaweza endelea kupokea taaria mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus


Share