Hatua kubwa yapigwa katika uzalishaji wa chanjo ya COVID-19

Majaribio ya chanjo ya COVID-19 yaanza katika Chuo cha Queensland

Majaribio ya chanjo ya COVID-19 yaanza katika Chuo cha Queensland Source: UNIVERSITY OF QUEENSLAND POOL

Majaribio ya chanjo ya COVID-19 kwa binadam yame anza jimboni Queensland, watu wa kwanza walio shiriki katika jaribio hilo walipokea chanjo zao jumatatu.


Miongoni mwa maelfu yawatu waliojitolea kushiriki katika jaribio hilo, 120 walichaguliwa na kunamatumaini kwa matokeo chanya ifikapo katikati yamwaka ujauo.

Watu hao walio jitolea kushiriki katika majaribio ya chanjo hiyo, kwa sasa wanakabiliana na miezi kadhaa yavipimo vya kila mara pamoja na uchunguzi wakaribu ambao hauta jumuisha wanasayansi tu bali, utajumuisha dunia nzima, itakayo watazama nakutumai matokeo chanya.


Share