Bw Habib Chanzi ndiye mwenyekiti wa Jumuiya yawatanzania wanao ishi jimboni Victoria, katika mazungumzo maalum punde baada yavizuizi hivyo kuondolewa, ali eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS hisia zake baada yakupewa uhuru ambao yeye nawakaaji wenza wa Victoria wametamani kwa muda mrefu.
Bw Chanzi aliweka wazi pia changamoto ambazo viongozi wenza na mamlaka husika, wanakabili kuhakikisha jamii zinaendelea kuwa salama wakati baadhi ya watu wame anza kufurahia uhuru wao mpya, na wakati huo huo mamlaka wanaripoti ongezeko ya idadi kubwa ya maambukizi ya Coronavirus kila siku.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.