Dhiki yatanda miongoni mwa wakazi wamiji ya mpaka wa Victoria na New South Wales

Jeshi la polisi lachunguza vibali vyamadereva wanao tumia mpaka wa Albury-Wodonga

Jeshi la polisi lachunguza vibali vyamadereva wanao tumia mpaka wa Albury-Wodonga Source: Amelia Dunn/SBS News

Mamlaka wamechukua hatua kali zakuzuia usambaaji wa virusi vya COVID-19 katika jamii kote nchini Australia.


Baadhi ya hatua hizo zimejuisha serikali za Victoria na New South Wales kuchukua uamuzi mgumu wakufunga mpaka wamajimbo hayo jirani.

Hata hivyo jamii zinazo ishi katika miji pacha ya mpakani ya Albury na Wodonga, wamejipata pahali pagumu wengi wao wakikosa bidhaa muhimu wanazo zihitaji upande wa pili wa mpaka na muhimu zaidi, uhaba wa taarifa kutoka kwa mamlaka umeongeza dhiki zaidi.

Bw Simba Musore ni mkaazi wa mji wa Albury, alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi yeye najamii yake walivyo pokea amri yakufunga mpaka huo, na jinsi maisha yamebadilika chini ya mazingira hayo mapya.


Share