Hata hivyo, watu binafsi pamoja na vyama vinavyo wakilisha jamii mbali mbali nchini, vimechukua hatua zakujaribu kuwa nusuru wanachama wa jamii walio jipata pabaya kwa sababu ya mlipuko wa janga la COVI-19 pamoja na hatua zakudhibiti janga hilo.
Deborah Kalei ndiye Rais wa shirika la KASA, shirika hilo huwakilisha nakuwahudumia wakenya wanao ishi Kusini Australia. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bi Kalei aliweka wazi aina ya misaada ambayo KASA ilitoa kwa wakenya walio athiriwa na janga la COVID-19. Kwa taarifa zaidi kuhusu KASA tembelea: kasa.org.au
Bonyeza hapo juu kwa usikize mahojiano kamili.