Swali ambalo litakuwa kwenye karatasi ya kura ni: “Pendekezo la Sheria: kubadili Katiba kuwatambua wa Australia wa Kwanza kwa kuanzisha Sauti yawa Aboriginal na wana visiwa wa Torres Strait. Una idhinisha badiliko hili lililo pendekezwa?”
Kama ilivyo tarajiwa, kura hiyo ya maoni ime zua gumzo za hisia mseto nchini kote. Wanachama wa jumuiya zawa hamiaji wanao stahiki kupiga kura na wanao unga pande mbili husika katika kampeni hiyo walichangia maoni yao tuki anza kwa wanao unga kampeni ya ndio.
Uta takiwa kujaza karatasi ya kura kwa majibu mawili “ndio” au “la” kwa ukamilifu katika kiingereza. Kupiga kura kwa raia wengi wa Australia wenye zaidi ya miaka 18 ni lazima, na unaweza kabiliwa kwa adhabu. Una ruhusiwa kupiga kura mara moja tu.
Australia ina majimbo sita, na ili kura hiyo ya maoni ipitishwe, lazima ikubaliwe na idadi kubwa ya wapiga kura katika majimbo mengi, hiyo ina maana angalau majimbo manne.
Ahadi ya kutambuliwa katika katiba ni sehemu ya hatua tatu inayo anza kupitia kura ya maoni na, ina endelea kujumuisha kusema ukweli pamoja na mkataba.
SBS ina tambua kuwa maoni yanayo wasilishwa katika makala haya, haya wakilishi maoni ya jumuiya pana na si uwakilishi wa takwimu ya umma wa Australia.