Alfred Koech afunguka kuhusu vizuizi vya ghafla Magharibi Australia

Alfred Koech

Alfred Koech balozi wa chuo cha Edith Cowan Source: Alfred Koech

Wakazi wa jimbo la Magharibi Australia wameishi, kwa muda mrefu bila vizuizi vyovyote vya Coronavirus tofauti na wenzao kote nchini Australia.


Ila, hali hiyo ilibadilika hivi karibuni, serikali ya jimbo hilo ilipotanganza vizuizi vya ghafla vya siku tatu baada ya kisa kipya cha maambukizi ya COVID-19 kutambuliwa jimboni humo.

Kujua jinsi jamii yawa Afrika wanao ishi mjini Perth walivyo pokea tangazo la vizuizi hivyo, Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na Alfred Koech ambaye ni Balozi wa wanafunzi katika chuo cha Edith Cowan mjini Perth, Magharibi Australia.

Bw Koech alizungumzia changamoto ambazo wanafunzi wakimataifa wamekabiliana nazo tangu janga la COVID-19 lilipoanza, na aina ya misaada inayo tolewa kwa waathiriwa wa janga hilo katika jamii yawakenya na jamii yawa Afrika wanao ishi Magharibi Australia kwa ujumla.

 


Share