Feature

Unawasiwasi kuhusu uraibu wa kamari wa mpendwa wako? Hivi ndivyo unaweza msaidia

Matokeo hasi kutoka kamari huja katika umbo nyingi, ziki athiri situ mcheza kamari bali familia nama rafiki zake pia. Iwapo mpendwa wako anakabiliana na uraibu wa kamari au yuko katika mchakato wakupona, kupata msaada ni mhimu. Nchini Australia, msaada huo unaweza patikana katika lugha kadhaa.

slot machines.jpg

Pokies present more risk of harm than any other form of gambling, according to an NSW Responsible Gaming Fund report. Credit: Getty Images/Alina555

Key Points
  • Potential harm from gambling extends from financial to mental health problems.
  • Family and friends are impacted by one’s compulsive gambling, but support is available.
  • Cultural sensitivities can prevent people from seeking help.
  • Helping a loved one effectively requires family and friends to get support too.
Hatari ya madhara mtandaoni na nje ya mtandao daima haiwezi onekana kila mara amesema Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Sydney Sally Gainsbury.
Mara nyingi huitwa uraibu wa siri kwa sababux, hauwezi uona katika macho ya mtu au kuunusa katika pumzi yao kama wanatatizo la kamari... Ila madhara ni yale yale, na gharama zakifedha ni zile zile.
Sally Gainsbury, Professor of Psychology at the University of Sydney.
Prof Gainsbury ni mkurugenzi wamatibabu ya kamari na kituo cha utafiti katika chuo hicho.

Amesema barabara yakupona kutoka kwa uraibu fiche wa kamari, ni mchako mgumu, kwa mtu anaye kabiliana na changamoto hiyo na, watu wakaribu yake.

Mara nyingi huwa kuna kurudi nyuma vile vile, amesema.
Tama ma lana kate talatupe.jpg
Online wagering tends to appeal to a different cohort than that of poker machines, but the harms are the same Credit: Getty Images/becon
7.2% ya watu wazima wako katika hatari ya madhara ya kamari.

Jamii zenye tamaduni na lugha tofauti (CALD) hazi shiriki zaidi katika kamari kuliko umma mpana ila, utafiti unaonesha kuwa wako hatarini zaidi kukabiliana na madhara ya kamari.

Natalie Wright, ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Uwajibikaji wakucheza Kamari jimboni New South Wales, amesema kuwa watu kutoka jamii tofauti wanao kabiliana na matatizo ya kamari, wana uwezekano wakuepuka kuomba msaada kwa sababu ya aibu na unyanyapaa.
Ushauri katika jamii nyingi ni kitu geni na dhana ya magharibi. Kwa hiyo, mara nyingi kuna dhana kuwa watu wanataka hifadhi vitu ndani ya jamii.
Natalie Wright, Director of the Office of Responsible Gambling in New South Wales
Sad family.jpg
Gambling harm doesn’t just affect the person who gambles Credit: Getty Images/uniquely India
Jamaa na marafiki wa watu wanao kabiliana na matatizo ya kamari, wanaweza athirika pia.

Mara nyingi huwa wanakabiliwa na matatizo yakifedha, yanayo husiana na matatizo ya kamari. Wanauwezekano wakukabiliwa kwa matatizo katika mahusiano yao na, lazima wakabiliane na madhara yake hasi.

“Kwa hiyo, watu wanastahili kuwa na msaada wao binafsi bila kujali kama, mhusika anajaribu kubadili uraibu wake wa kamari. Ni vizuri pia wakati wanajaribu kumsaidia mtu ambaye anajaribu kupona,” Prof Gainsbury ame elezea.
Concerned man with bill.jpg
Changes in someone’s financial wellbeing can be a sign their gambling has become an issue. Credit: Getty Images/Narisara Nami
Adam*, ni mkaaji wa Magharibi Sydney kutoka jamii yakiarabu, amekuwa katika mchakato wakupona kutoka uraibu wa kamari tangu 2014.

Amesema familia yake ya karibu iliathirika pia na, daima wame kuwa wakimsaidia katika safari yake ya uponaji.

Anakumbuka jamaa wake wa karibu akitafuta msaada kwake binafsi, kupitia washauri wakati alipokuwa katika mchakato wakupona.

“Waliweza mudu mahitaji yangu ya uponaji, ambayo wakati mwingine yalikuwa magumu kuelewa kama wewe si mraibu. 

“Nadhani kupata msaada wakitaalam kuliwapa uelewa kuwa, hawana wajibu kwa kilicho tokea. Hawana kosa kwa kilichokuwa kinatokea, hawana kosa kwa kinacho fanyika. Na wanaweza nielewa kwa urahisi kama mtu binafsi kwa urahisi.”

Kwa Adam, mageuzi kwa safari yake ya uponaji ilikuja kupitia shirika la , ambalo ni kundi la wanaume na wanawake wanao changia uzoefu wao na husaidiana kupona kutoka matatizo ya kamari.

Ila Adam ana amini kila mtu ana njia tofauti yakupata vifaa vyaku kabiliana na matatizo ya kamari.
[Baadhi ya] watu hufanikiwa kwa kuenda kupewa ushauri kilawiki, kubadili ajira, kubadili miradi ya maisha au kufanya mazoezi zaidi. Kuna vitu ambavyo vinaweza tumika kwa kila mtu.
Adam*, recovering from problem gambling
support group.jpg
Peer-to-peer support and online forums can be helpful for some. Credit: Getty Images/Marco VDM
Mbinu yoyote ya msaada inaweza kuwa nzuri, kama msaada unaofaa unatolewa, amesema Prof Gainsbury.

Ame linganisha kukabiliana na matatizo ya kamari, na hali ya dharura ndani ya ndege, ambako abiria hushauriwa kuvaa barakoa yao kabla yakuwasaidia wengine.
Ni mhimu kwa watu kutambua kuwa, kuna msaada mwingi wanao weza pata, hawako wenyewe... [na] wawe makini kwa usemi wakuvaa kwanza barakaoa yako ya oxygen.
Professor Gainsbury.
Doctor with patient.jpg
Some people feel more comfortable asking their doctor to direct them to a specialised service. Credit: Getty Images/nahsoon
Huduma zilizo jimboni, hutoa rasilimali na ushauri kwa simu, mtandaoni au ana kwa ana.

Kampeni ya serikali ya New South Wales (NSW) kwa jina la , ina lengo lakuwasaidia watu kutoka jamii zenye tamaduni tofauti ambazo, zina kabiliana na matatizo ya kamari na hazina uhakika wa jinsi yakupata msaada.

Sehemu yakwanza kwa mtu yeyote anaye hitaji msaada jimboni NSW ni kupitia namba hii 1800 858 858. Tovuti yao imetafsiriwa katika lugha tano za jamii, lugha hizo zikijumuisha Kiarabu, kichina rahisi nachakitamaduni, Kihindi, kikorea na kivietnamu.

Ushauri wakifedha unaweza tolewa pia.

Kama kuna madeni yanayo ongezeka kwa sababu ya kamari ya mpendwa wako, au kuna maswala yakifedha unaweza tafuta ushauri wakifedha Bi Wright amependekeza..
Watu wengi wata tafuta msaada usio rasmi. Kwa hiyo, kama itakuwa kutoka mtaalam wa afya, au msaada ndani ya jamii kama, viongozi wa jamii au viongozi wakidini, au msaada ndani ya familia.
Professor Gainsbury.
“Ushauri katika zaidi ya lugha 50, hutolewa kwa kila mtu kote jimboni,” amesema Bi Wright.

Mwishowe, amesema kutoa msaada kwa mtu ambaye anatatizo la kamari, kuna enda sambamba naku wahamasisha kutafuta msaada wakitaalam.

*Si jina lake halisi.

Kwa msaada, piga simu au bonyeza kwenye viungo hapo chini.


Share
Published 23 October 2022 6:20pm
By Zoe Thomaidou
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends