KEY POINTS:
- More than 17 million Australians are registered to vote in the referendum later this year.
- The passage of the Voice referendum bill triggers the process of setting a firm date for the vote.
- The date must be set within two months and six months from today.
Wa Australia watapiga kura rasmi kwa kura ya maoni ya the Voice to Parliament katika miezi sita ijayo, baada ya muswada waku ashiria kura hiyo ya maoni kupitishwa ndani ya Seneti kwa kura 52 dhidi ya 19.
Bunge ili ruka kiunzi chake cha mwisho rasmi kabla ya kura ya maoni Jumatatu, wa Australia sasa wanatarajia kuamua kama wata weka the Voice kiungo mhimu cha 2027 cha Uluru Kauli ya kutoka Moyoni- ndani ya katiba.
Wanaharakati wa kambi ya 'Ndio' wamesema "wamesema kazi ya bunge ime kwisha", mjadala huo sasa uta ongozwa na wanaharakati wa mashinani kwa mageuzi ya katiba.
Waziri wa waAustralia wa asili Linda Burney amesema maendeleo hayo yame ileta Australia "hatua moja karibu" kuwatambua wa Australia wa asili ndani ya Katiba nakufanya "nchi nzuri kuwa bora zaidi".
"Imekuwa ... Leo, mjadala wakisiasa ume kwishwa. Leo, tunaweza anza mjadala wakitaifa kwa kiwango cha jamuia," alisema.
"Kwa muda mrefu, wa Australia wa asili wame kuwa katika hali mbaya kuliko jamii zingine nchini Australia. Ni mfumo ambao umevunjika. Na the Voice ni fursa yetu bora, kuikarabati kwa sababu tunapo sikiza watu mashinani, pamoja nakushauriana na wenyeji, huwa wana fanya maamuzi bora nakupata matokeo bora."
Chama cha Labor kimesisitiza kuwa the Voice itakuwa tume la ushauri, likiwapa wa Australia wa asili fursa yaku shauri bunge na serikali kwa maswala hususan yanayo waathiri.
Ila baadhi yawakosoaji wayo wamedai kuwa pendekezo hilo lina hatari nyingi wakati wengine wame sisitiza tume haiwapi watu wa asili mamlaka yakutosha.
Kura ya maoni ya kwanza katika karibu robo ya karne, itakuwa kati ya miezi mbili na sita kutoka Jumatatu, hata hivyo Waziri Mkuu Anthony Albanese ame dokeza itakuwa mwaka huu.
"Fursa hii ya mara moja katika maisha kiunua taifa letu juu zaidi," alisema.

Independent Senator Lidia Thorpe reacts after the passing of the Voice to Parliament in the Senate chamber at Parliament House. Source: AAP / Lukas Coch
"Hii ni fursa yakufanya vitu kwa ubora, badala yakufanyia vitu wa Australia wa asili, kufanya mageuzi pamoja nawa Australia wa asili."
Chama cha mseto chapitisha muswada wa kura ya maoni
Licha yakupinga the Voice, chama cha Mseto kime pitisha muswada huo asubuhi ya jamatatu.
Waziri kivuli wa chama cha Liberal Michaelia Cash, alisema kura ya Ndio, ita"badilisha bila uwezo wakurekebisha" katiba ya Australia, alidai pia kuwa chama cha Labor, kimefeli kutoa taarifa yakutosha kwa jinsi tume hiyo 'inayo zua 'mgawanyiko' itafanya kazi.
"[Ila] tuna imani kwa watu wa nchi hii, na haki yao yakutoa maoni yao kwa swala hili," alisema.
"Haijulikani, inagawanya, na itadumu. Kama haujui jinsi tume ya the Voice itafanya kazi, maoni yangu ni: piga kura ya La."
Jacinta Price ni msemaji wa maswala yawa Australia wa kwanza katika chama cha mseto. Bi Price ni mwanamke kutoka ukoo wa Warlpiri/Celtic, amesema kuachia bunge jukumu laku shughulikia maelezo kamili baada ya kura ya maoni, ni jambo linalo jawa hatari zaki sheria.
"Waziri Mkuu anataka tumuamini bila kuhoji aki tia saini cheki yake ambayo ni tupu, na turuhusu pendekezo lake hatari liwekwe milele ndani ya katiba wakati hawezi toa dhamana yoyote," alisema.
Wabunge wachache wa chama cha mseto walipiga kura dhidi ya muswada huo, hatua yakiufundi itakayo waruhusu wachangie kwa kesi ya La, katika vijitabu rasmi vya kura ya maoni vitakavyo tumwa kwa wapiga kura.
Chama cha Greens chakaribisha 'siku ya kihistoria'
Msemaji wa chama cha Greens kwa watu wa asili wa Australia Dorinda Cox, ambaye alifanya mwafaka kwa mapendeleo yake kwa Mkataba na Ukweli vije kabla ya Voice, aliashiria "Siku ya kihistoria" kwa wa Australia wa kwanza.
"Kazi ya bunge ime isha. Ni wakati wa kampeni ya Ndio mashinani, kuenda katika jamii nakuchangia na wa Australia wote kwa nini kura hii ya maoni ni mhimu, na kwa nini Voice to Parliament ni mhimu sana," alisema.

Ms Burney, seated left, was present for the debate. Source: AAP / Lukas Coch
Kama vile Seneta Cox alivyo sisitiza, the Voice haita dhoufisha uhuru wa watu wa asili, hotuba yake ili ingiliwa mara kadhaa na seneta huru Lidia Thorpe, aliye jiondoa katika chama cha Greens kufanyia the Voice kampeni huru.
"I thibitishe!" Seneta Thorpe alisema mara kadhaa.
Lidia Thorpe akosoa Voice 'bandia na kujifanya'
Seneta Thorpe, ni mwanamke wa ukoo wa DjabWurrung, Gunnai na Gunditjmara, ali elezea Jumatatu kuwa ni "siku ya unyabulishaji" na ali wahamasisha wa Australia wa susie kura hiyo ya maoni.
Alipo simama kuongea, Seneta Thorpe ali elezea muswada huo kama "msumari wa mwisho katika jeneza", ila bado haja sema ata pigia kura upande gani wa kura hiyo ya maoni yeye binafsi.
"Nita piga kura ya La kwa wazo hili baya ambalo hali tupi mamlaka," alisema.
"Ila siwezi unga mkono kitu ambacho haki wapi watu wangu mamlaka. Siwezi unga mkono kitu ambacho kime chaguliwa na mtu yeyote ambaye yuko mamlakani."

Minister for Indigenous Australians Linda Burney poses for a photo with 40 members of Jawun at Parliament House in Canberra. Source: AAP / Mick Tsikas
"Ndio, niko hapa kuupenyeza, kuzua rabsha na kuvuruga ubabe wa wazungu unao wakilishwa humu."
Seneta Thorpe, aliyevaa shati iliyo kuwa ime andikwa 'Gammin' wakati wa mjadala huo, alitaka Bunge itekeleze mapendekezo kutoka Tume ya Kifalme kwa vifo vya wa Aboriginal gerezani.

Independent senator Lidia Thorpe reacts during debate on the Voice to Parliament in the Senate chamber at Parliament House. Source: AAP / Lukas Coch
"Tuna sikia hizi hadithi zote nzuri kuhusu jinsi hili lita karabati maisha yetu. Ita tatua kila kitu. Hatuwezi fanya chochote hadi baada ya kura ya maoni... Wakati huo huo, watoto wana teswa ndani ya magereza."
Alipo zungumza wakati wa mjadala Jumatatu, mbunge wa chama cha Labor Malarndirri McCarthy ali wahamasisha wa Australia wapiga kura ya ndio "kwa siku bora za usoni" na alisema the Voice itakuwa na "maana kubwa" kwa watu wa asili.
"[Watu wa asili] wana wahamasisha wa Australia wote, wahisi fahari ya wakati huu katika historia ya nchi yetu, ambako tunaweza inuana," alisema.
"Ambako jamii zawa Australia wa kwanza, zinaweza kuwa nakuhisi wako sehemu ya nchi hii."
Wasiwasi kuhuhu mwelekeo baada ya madai ya Pauline Hanson
Baada ya Seneta wa chama cha One Nation Pauline Hanson, kuwa hamasisha wa Australia “waulize kwa nini” vizazi vilivyo ibiwa vilitokea, Seneta McCarthy alikiri ana wasiwasi kuhusu mwelekeo wa mjadala huo katika miezi ijayo.
Seneta McCarthy ali wahamasisha wa Australia “wasikize sehemu bora zao binafsi” katika mjadala huo.
“Nina wasiwasi mdogo, ninapo sikia baadhi ya madai yanayo tolewa, ” alisema.

Senator McCarthy conceded concern over the tenor of the debate, just moments after Pauline Hanson's (pictured) comments. Source: AAP / Lukas Coch
“Hapo ndipo tunaweza pata nafsi zetu bora kama nchi, sehemu bora yetu kama wa Australian.”
Seneta Hanson awali alikuwa amedai kuwa watu wengi katika Vizazi Vilivyo ibwa, “hawange pona” bila kuondolewa katika familia zao.
“Unajua, unaweza zungumza kuhusu Vizazi vilivyo ibwa. Ilitokea wakati huo. Jiulize kwa nini,” alisema.
Ripoti mhimu ya 1997 Kuwaleta Nyumbani ilipata kuwa kuondolewa nyumbani kwa watoto wajamii zawatu wa asili, ili kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadam, na kulikuwa na uwezekano mkubwa wajukuu wa watoto hao walio ondolewa makwao wanaweza fungwa jela, kuwa na matatizo yaki afya, na kuwa na uwezekano mdogo wakupata ajira.
Bw Albanese alisema alikuwa haja ona madai ya Seneta Hanson ila, alidhani yana ambatana na vitu alivyo wahi sema katika siku za nyuma.
“Sina nia yaku yajibu kwa sababu, sidhani yana stahili pewa jibu la waziri mkuu. Nita omba pawe mjadala wa heshima kila sehemu,” alisema.
“Bila kujali jinsi watu watapiga kura, wanaharakati wanastahili fanya wawezavyo, kusema ukweli, siku sema vitu ambavyo wanajua si kweli.”
Linda Burney amesema Voice italeta mabadiliko ya kimuundo
Kura za maoni hupitishwa na wengi, jumla ya sehemu kubwa ya wengi katika majimbo. Wakaaji wa NT na ACT hawa jumuishwi katika hesabu hiyo.
Seneta huru David Pocock alisisitiza kuwa wakaaji wa ACT na NT hawana kura sawia na wenzao.
Seneta Pocock ali elezea majaribio ya chama cha mseto, kusema kuwa kura hiyo ya maoni ni "Canberra Voice" kuwa ni "si kweli kabisa".
"Haya ni matokeo ya moja ya mchakato mkubwa wa ushauriano katika historia ya Australia.... Ndio, kama hakija vunjika, usi fanye ukarabati. Ila kama kime vunjika, kina hitaji karabatiwa. Hii ni fursa yakufanya ukarabati," alisema.
Sauti yawatu wa Asili Bungeni, ilikuwa moja ya ombi la iliyo tolewa na viongozi wa jamii zawatu wa asili 2017.
Wa Australia wata ombwa baadae mwaka huu, katika kura ya maoni wapige kura ya Ndio au La, iwapo wana unga mkono mabadiliko katika katiba kuunda tume yakudumu ndani ya bunge na serikali ya shirikisho itoe ushauri kwa maswala yanayo wa athiri wa Australia wa kwanza.
Uamuzi na taarifa kamili ya mfumo vita amuliwa na wabunge bungeni, kambi ya Ndio ya kura hiyo ya maoni ikishinda.
Bi Burney amesema ana amini pendekezo hilo, lita kuwa kitu kinacho hitajka kulenga afya duni, matokeo ya kijamii nakiuchumi pamoja na matarajio ya matokeo ya maisha ambayo wa Aboriginal na watu wa visiwa vya Torres Strait hupitia.
Maelezo mapya kwa malengo ya Kuziba Pengo, inayo fuatilia pengo kati ya wa Australia wa asili na jamii zingine kwa afya, vipimo vya kijamii na ustawi wiki jana ilionesha ni .
"Inaleta mageuzi yaki muundo na itasogeza mjadala kwa maswala kama kuziba pengo," alisema.
"Mamlaka yako ndani ya kanuni, ni mamlaka mhimu ya maadili kuanzia. Fikiria kanuni: itakuwa huru, na itatoa ushauri huru situ kwa bunge ila pia kwa serikali ya shirikisho.
"Itawajibika. Itakuwa na usawa, ita ongozwa na jamii na itakuwa ndani ya miundo na mashirika yaliyopo kwa sasa."
'Ondoa urasimu ndani yake'
Kiongozi wa chama cha Nationals, David Littleproud, alisema Novemba mwaka jana kuwa chama chake kita fanya kampeni ya kura ya La kwa Voice to Parliament.
Wakati huo alisema haku dhani pendekezo hilo "lita funga pengo kwa dhati".
Aliongezea kuwa bado ana shikira msimamo huo na ana amini suluhu hai hitaji mageuzi ya Voice to Parliament kuwekwa ndani ya katiba.
"Serikali zime mwaga mabilioni ya dola kujaribu kutatua [kufunga pengo] ila, tume ifanya vibaya," ali eleza redio ya ABC.
"Lengo la usawa daima lime kuwa hapo, ni utendaji tu," alisema, aki kiri kuwa chama chake ndani ya serikali ya mseto kwa zaidi ya miaka 12 kili kuwa sehemu ya tatizo katika mwelekeo uliofeli.
"Tuli feli. Siogopi kusema kuwa serikali za kila aina zime feli... uki ondoa urasimu ndani yake, tunaweza funga pengo."
Aliongezea kuwa jibu lina husu suluhu kwa kiwango cha jamii, bila mahitaji ya kuwa na tume ya Voice to Parliament.
"Hapo ndipo wazee katika jamii, si kiwango cha kanda, wanastahili shirikishwa nakuwezeshwa... Inahusu kuwaondoa warasimu Canberra na, kuwaweka ndani ya vyumba vya mikutano ya jamii, sehemu za nje ambako watu wana ota moto, nakuwasikiliza wazee."