hutambua watu wanao pewa kipaumbele na, sehemu kote nchini ambako chanjo zinatolewa. Wafanyakazi wa afya ambao wako katika mstari wa mbele, wafanyakazi wa karantini na mipaka, pamoja na wakaaji katika makazi ya huduma ya wazee na ulemavu, pamoja na wafanyakazi ni miongoni mwa watu ambao wamepewa kipaumbele katika mkakati huo wa utoaji.
Kujua kama unaweza pata chanjo ya COVID-19 na wapi unaweza omba miadi tembelea
Kama una umri wa miaka 40 au zaidi unastahiki kupata chanjo. Baadhi ya watu wenye kati ya miaka 16 na 39 wanaweza stahiki pia kupata chanjo.
Kama hau stahiki na una miaka 18 au zaidi, unaweza omba kujulishwa unapo stahiki.
Watu wenye chini ya miaka 16, bado hawastahiki kuchanjwa nchini Australia.
Unaweza omba miadi kwa GP wako nakupata taarifa kuhusu, chanjo katika lugha yako:
Je! ni chango gani zinazo pendekezwa?
Kundi la ushauri lakiufundi kwa kwanjo nchini Australia (ATAG) limependekeza chanjo ya COVID-19 Comirnaty (Pfizer) kama chanjo inayo pendelewa kwa watu wenye kati ya miaka 16 na 56.
Chanjo ya COVID-19 AstraZeneca, nayo inaweza tolewa kwa watu wenye kati ya miaka 18 hadi 59.
Utoaji wa chanjo ya Coronavirus nchini Australia

taarifa ya chanjo ya COVID-19 Source: SBS
Idara ya Afya ya Australia
Kipaumbele cha umma kwa chanjo ya Coronavirus (Australia)
Chanjo yako itahifadhiwa katiak kumbukumbu ya umma
Serikali lazima ihifadhi baadhi ya taarifa kuhusu watu ambao wame chanjwa, kwa ajili yaku weza kujua nani ameipata. Ni jukumu la wanao toa mradi wa chanjo ya Australia, kusajili taarifa ya kila mgonjwa anaye pokea kila chanjo ya COVID-19.
Taarifa kuhusu hali ya chanjo ya mtu binafsi, inatarajiwa kupatikana kupitia My Health Record, Medicare (Taarifa ya historia ya chanjo), au cheti kitakacho chapishwa wakati wa chanjo, ikifuatwa na kumbukumbu yaki elektroniki kupitia barua pepe.
Viwango vya chanjo vita tofautiana
Inachukua wiki mbili kwa mwili kuanza kuunda kinga zakujilinda dhidi ya virusi ila, "ulinzi" huo haumaanishi ‘kinga’. Dkt Kylie Quinn ni mtaalam wa kinga katika chuo cha RMIT, alielezea SBS aina ya viwango tofauti vya ufanisi wa chanjo:
Kiwango cha 1 - zuia maambukizi kabisa
Kiwango cha 2 - kutoweza kuzuia maambukizi ila, inaweza zuia kusambaa nakusababisha ugonjwa
Kiwango cha 3 - kutoweza kuzuia ugonjwa ila, hai endelei kuwa ugonjwa mubaya.
Chanjo zote za COVID-19 zinatolewa bure
Chanjo zina tolewa bure kwa raia wote wa Australia, wakaaji wakudumu na watu kila mtu mwenye viza. Mtu yeyote nchini Australia ambaye ana viza ya uanafunzi, kazi, ujuzi, familia, uchumba, mkimbizi, muomba hifadhi, viza ya ulinzi ya muda, viza yakibinadam, kanda, viza ya mpito au viza maalum, ana stahiki kupokea chanjo ya COVID-19 bure.
Watu ambao wako vizuizini nao pia wanastahiki, pamoja na watu ambao viza zao zimefutwa.
Taarifa ya Serikali kuhusu Coronavirus
- Idara ya Afya - taarifa ya chanjo ya COVID-19 .
- Idara ya maswala ya nyumbani - taarifa ya COVID-19 .
- Watu nchini Australia lazima wabaki angalau mita 1.5 mbali na wengine
- Ukihisi dalili za mafua, baki nyumbani na fanya mpango waku pimwa
- Tafadhali chunguza mwongozo unao faa kwa jimbo au mkoa wako: , , , , , , .