KEY POINTS:
- Anthony Albanese has unveiled the wording of the Voice referendum.
- Australians will head to the polls at the end of this year.
- Mr Albanese has revealed fresh details on how the body would function.
Wa Australia sasa wanajua maneno watakayo soma wakati wa kura ya maoni ya .
Umma utapiga kura katika kura ya maoni ya kwanza katika karibu nusu karne, na ikifanikiwa itakuwa mara ya kwanza wa Australia watakuwa wamepiga kura kubadilisha katiba yao tangu 1977.
Akizungumza baada ya mkutano na kikundi cha kazi cha kura ya maoni ya Voice Alhamisi, Waziri Mkuu Anthony Albanese aliweka wazi swali litakalo chapishwa kwenye karatasi ya kura:
A proposed law: to alter the Constitution to recognise the First Peoples of Australia by establishing an Aboriginal and Torres Strait Islander Voice. Do you approve this alteration?
Sasa swali hilo lita pelekwa bungeni kupigwa mhuri, kabla wa Australia waelekee katika vituo vyakupiga kura mwisho wa mwaka.
The Voice inaweza fananaje?
The Voice itakuwa tume litakalo shauri serikali kuhusu maswala yanayo athiri jamii zawa Australia wa Kwanza. Tume hilo halitakuwa na mamlaka yakupinga sheria.
Bw Albanese aliweka wazi pia taarifa mpya kuhusu, jinsi tume hiyo itafanya kazi, alisema:
- Wanachama watakuwa na mihula yakuhudumu "kuhakikisha uwajibikaji"
- Itakuwa na usawa wa jinsia na itawajumuisha vijana pia
- Itawajumuisha wawakilishi kutoka majimbo yote na wilaya
- Itajumuisha wawakilishi kutoka jumuia maalum za vijiji vya mbali
Ila hakutaka jadili kama wanachama watachaguliwa kidemokrasia au wata teuliwa.

The question is slightly different to the draft wording Mr Albanese unveiled at the Garma festival last year. Source: AAP / Aaaron Bunch / AAP Image
Ni hatua gani zitakazo fuata?
Kura bungeni, kisha kura ya wananchi.
Kwa kura ya maoni kufanyika, muswada lazima upitishwe bungini.
Hata hivyo kitu kisicho cha kawaida, si lazima muswada huo upitishwe ndani ya Nyumba yawa wakilishi na Seneti. Kinadharia inaweza pita ndani ya Nyumba ya Wawakilishi ambayo inawabunge wengi wa chama cha Labor mara mbili, kwa maana kwamba muswada huo unakuwa na dhamana yakufanikiwa.
Watuwazima wa Australia wata takiwa kupiga kura ya "Ndio" au "La" kwa swali ambalo Bw Albanese aliweka wazi Alhamisi.
Wapiga kura wengi katika majimbo mengi, wanahitajika kufanya the Voice kuwa kweli.
Kizingiti hicho kiki fikiwa, Bw Albanese amesema mchakato na jamii yawa Australia wa asili pamoja na umma mpana uta anza ku "tekeleza muundo wa the Voice".
Punde hilo litakapo fanyika, itapelekwa bungeni kama sheria yoyote nyingine, kujadiliwa nakufanyiwa tathmini.
Tuna tarajiwa kupiga kura lini?

Bw Albanese ame ahidi mara kwa mara kuwa kura hiyo itafanywa kufikia mwisho wa mwaka huu.
Mwezi uliopita alipunguza muda huo zaidi tena, alidokeza kuwa umma uta elekea debeni kati ya Oktoba na Disemba.
Kura za maoni hufanywa Jumamosi, kumaanisha kuna tarehe chache tu ambazo kura hiyo inaweza fanywa.