Key Points
- Victoria to set up a new pandemic preparedness centre
- Australia to provide $31.5 million for finding new ways to treat COVID-19
- A new study shows Paxlovid lowers hospitalisation and death risks in older people
Jumatano, Australia iliripoti vifo 65 vya UVIKO-19, 26 vikiwa Victoria, 22 New South Wales na 10 Queensland.
Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, idadi ya wanao lazwa hospitalini na vifo nchini Australia .
Mkutano wa baraza la mawaziri wataifa unaendelea kuamua kama muda wakujitenga kwa kesi chanya za UVIKO-19 unaweza punguzwa kutoka siku saba hadi siku tano.
Chama cha wafanyakazi wa huduma za afya, kina amini muda wakujitenga unstahili futwa kabisa.
Victoria itatoa uwekezaji wa $75 milioni kwa chuo cha Melbourne kwa kuanzisha kitengo kituo kipya cha maandalizi ya janga.
Mfadhili na mfanyabiashara kutoka Canada, Geoffrey Cumming ata toa $250 milioni kwa kituo hicho. Huo ni mchango mkubwa zaidi wa ufadhili ambao umewahi tolewa kwa utafiti wamatibabu nchini Australia.
Australia itatoa $31.5 milioni kwa watafiti kupata mbinu mpya zakutibu UVIKO-19 nakuelewa madhara yake ya muda mrefu.
Australia imevuka idadi ya kesi milioni 10 za UVIKO-19. Kuanzia saa tisa mchana ya 30 Agosti 2022, maambukizi 10,018,025 ya UVIKO-19 pamoja na idadi ya vifo 13,834, vimeripotiwa nchini.
Umri wakati wa kesi zote na vifo ni miaka 31 na miaka 83.
Utafiti mpya kutoka Israel uliochapishwa katika jarida la matibabu la New England, umeonesha kuwa kidonge cha Paxlovid hupunguza hatari yakulazwa hospitalini kwa 73% na vifo kwa 79% katika watu wenye miaka 65 na zaidi.
Pata zahanati ya UVIKO
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo yako ya kipimo cha RAT hapa, kama matokeo yakipimo ni chanya
Soma kuhusu taarifa ya UVIKO-19 katika lugha yako kwenye