Nyuma ya namna tofauti ambazo watu binafsi na vikundi huchagua kufafanua Januari 26, kiini cha swala la uhuru, ambayo inamaanisha uwezo wakujitawala kwa wa Australia wakwanza kwa ardhi zao, elimu, sheria, sera, afya na kadhalika, ilivyokuwa kabla yakuwasili kwa wazungu na haikuwahi tolewa.
Kuna makubaliano mapana kuhusu dhana ya uhuru kwenye kiini cha mjadala wa haki zawa Aboriginal, na wanavisiwa wa Torres Strait. Hata hivyo, miongoni mwa vikundi vya wa Australia wa kwanza, kuna maoni tofauti kuhusu jinsi Uhuru unatambuliwa.
Hii ni sehemu yakuanzia kwa mjadala wa umma wa Australia kuhusu Kutambuliwa, Mkataba, Sauti na Ukweli. Maoni hayo tofauti yame undwa na mifumo tofauti yakutambuliwa kwa wa Australia wa kwanza ambayo Australia inajadili.

Wa Australia washerehekea siku kuu ya Australia, wakati mjadala unaendelea kuhusu kubadili siku hiyo Source: Getty Images
‘Kutambuliwa’
Moja ya njia ya Kutambuliwa nikubadili katiba ya Australia, iwatambue wa Australia wa kwanza. Kazi 2020 yakubadili katiba ina ungwa mkono na orodha ndefu ya japo lawataalam, chunguzi za Seneti, tume zakatiba, baraza za kura za maoni, ripoti na mapendekezo yaliyo tolewa tangu miaka ya 1980.
Moja ya mifumo maarufu zaidi katika mstari wa mbele wa majadiliano haya ni ‘’, taarifa hiyo ime elezewa kuwa ni kelele cha mazungumzo 13 katika muda wa siku tatu, yaliyo fanywa kote nchini na wawakilishi wa jamii zawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait.
Dean Parkin, ni Mkurugenzi wa From the Heart, ambayo ni kampeni yakuhamasisha umma kuhusu Taarifa ya Uluru. Amesema wanafanya kazi kupata msaada kutoka umma, kuunga mkono kwa sauti bungeni.
"Jukumu letu ni asilimia 100 kwa Taarifa ya Uluru. Kwa hiyo kuelezea ukweli wa mkataba, sehemu ya ajenda yetu na nilivyo sema ndani yake kuna, wazo la sauti bungeni, inayo wakilisha watu wajamii yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait nakuzungumza bungeni, inazungumzia demokrasia ya Australia na inakinga ya katiba ya Australia, ili isiweze futwa kama mashirika mengine katika siku za nyuma."
‘Sauti’
Lengo lakuwatambua wa Australia wa kwanza ndani ya katiba, nikuwapa 'Sauti' ambayo itawawezesha kuwa na ushawishi nakufanya maamuzi kwa maswala yanayo husu jamii zao.
Ila baadhi wanadhani kuwa 'Sauti' hiyo inaweza patikana kwa kuunda tume ya uwakilishi ambayo, inaweza kuwa 'Sauti ya serikali' badala ya 'Sauti ya Bunge', kama ilivyo dokezwa na waziri wa waAustralia wa Kwanza, Ken Wyatt.
“Ukweli ni kwamba unaweza kuwa na sauti bungeni ila, sauti kwa serikali ni kwa chama ambacho kime unda serikali, wao ndiwo wenye mikoba ya bajeti, wao ndiwo wana tengeza sera, wao ndiwo wana wasilisha miswada.
“Kwa hiyo hao ndiwo unastahili shawishi, ni serikali. Sauti kwa bunge inakuja kutoka kwa sauti kwa serikali," alisema Bw Wyatt.

Minister for Indigenous Australians Ken Wyatt speaks to the media during a press conference at Parliament House in Canberra, Tuesday, August 17, 2021. Source: AAP Image/Lukas Coch
Ila, kwa mwanamke kutoka jamii yawa Bundjalung na Kungarakan, Dani Larkin, pendekezo la Bw Wyatt kuwa na tume lakisheria badala yakulijumuisha ndani ya katiba, yatakuwa matokeo mabaya naya kukatisha tamaa.
"Kume kuwa msaada mwingi kuendeleza sauti hiyo bungeni kwa kura ya maoni ya katiba, ili iweze lindwa dhidi yakuzimwa, na kuondolewa kwa ishara ya kalamu. Nadhani hayo yanaweza kuwa matokeo mabaya nayakusikitisha kwa watu ambao, wamefanyia swala hili kazi nyingi ila zaidi kwa wazee, alisema.
‘Mkataba’
Dhana nyingine ambayo imejadiliwa kwa upana ni 'Mkataba', yenye maana ya makubaliano rasmi kati ya serikali na jamii zawa Australia wa kwanza, inayo tambua uwepo wa jamii zawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait kabla ya ukoloni wa Uingereza na, kuchukuliwa kwa ardhi nakutawanywa kwa jamii zawa Australia wa kwanza. Kwa wengi, mkataba wakitaifa au wamajimbo au mikataba katika maeneo ya kikanda (badala ya Sauti kwa Bunge) inastahili kuwa lengo la kwanza, kwa sababu inamaanisha kutambuliwa kwa uhuru na mwanzo wa upatanisho nakusema ukweli kama vile mataifa ya New Zealand, Marekani na Canada yalivyo fanya na jamii zawatu wao wa Kwanza.
Ndiyo sababu kundi la wa Australia wa kwanza, walijitoa katika kongamano la Uluru la 2017, mjumbe kutoka jamii yawa Gunnai na Gunditjmara kutoka Victoria, Lidia Thorpe, kwa sasa ni seneta wa Victoria anaye wakilisha chama cha Australian Greens.

Senator Lidia Thorpe during a smoking ceremony at the Aboriginal Tent Embassy at Parliament House in Canberra. Source: Getty Images
Ana amini bado panastahili kuwa mchakato jumuishi wa ushauriano, kwa kila ukoo na taifa.
"Ni haki yao kuamua wanachotaka na wanacho hitaji. Nadhani tunastahili hakikisha tunafanya mazungumzo na watu kwa heshima, nakuwaruhusu watu, watu wote waje mezani na situkio tu la walio alikwa linalo wafungia nje watu wetu wengi wa mashinani. Bi Thorpe alisema.
Kwa swala la uhuru, wanaharakati wa mashinani kwa muda mrefu wamekuwa mhimu katika kampeni yakuboresha, maisha yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait.
Baadhi ya vikundi vya vijana waki Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait Islander, vinapendelea dhana ya mkataba na vinapinga wazo la kura ya maoni au kutambuliwa ndani ya katiba, kwa sababu inaweza kuwa na maana yakushiriki katika mifumo yakikoloni ambayo wamekataa kutambua. Kwa mtazamo wao, kuna mgongano kati ya mamlaka yakikoloni na, uhuru wa watu wa asili, pamoja na haki yao yakujiamulia.
Kundi hizo za vijana zina unda mtazamo wakisiasa kupitia intanet, mitandao yakijamii, pamoja nakuratibu, kuhamasisha nakuongoza maandamano mitaani wakiomba mageuzi.
Katika mstari wa mbele dhidi yakutambuliwa kikatiba, kuna kundi kwa jina la Warriors of the Aboriginal Resistance, kundi hilo hujulikana pia kwa ufupi kama WAR.
Boe Spearim ni mwanaume kutoka jamii yawa Gamilaraay, Kooma na Muruwari, yeye ni mwanachama wa kundi hilo la WAR. Amesema kundi hilo daima limepinga mwelekeo huo "wakutoka juu kushuka chini.” Ameongezea kwamba:
“Nadhani walikuwa wakijadiliana na jamii katika hali isiyo sahihi, na pia sisi wa Aboriginal hicho si kitu tulikuwa tukitafuta, au kutaka kujadili pia. Mkataba ulikuwa mezani na daima ulikuwa sehemu ya majadiliano.”

Indigenous activists and supporters protesting in Melbourne on 26 January 2019. Source: Getty Images
Msimamo rasmi wa kundi la WAR nikuto shiriki katika mifumo yakikoloni ila, Bw Boe ana elewa umuhimu wa kujitawala, unawaruhusu wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait Islander kufanya maamuzi yao katika hali hiyo.
Kuna mjadala pia kuhusu jinsi mafanikio yana fanana, kwa upande wakutambuliwa.
Michael Mansell anatoka katika jami yawa Palawa. Bw Mansell ni mwanaharakati, mwanasheria, yeye pia ni mwenyekiti wa wa baraza la ardhi lawa Aboriginal wa Tasmania. Ana amini kwamba watu waki Aboriginal wana uamuzi wakufanya kati yakutambuliwa kwa maana au kutambuliwa ki ishara tu.
"Kutambuliwa kiishara ni aina ya kitu kilichofanyika katika mwaka wa 2007, Kevin Rudd alipo omba msamaha kwa vizazi vilivyo ibiwa, Bw Mansell alisema.
Bw Mansell ame elezea jinsi anaweza pata utambulizi wa maana kwa wa Aboriginal.
“Si mchakato mgumu kama mkataba unawasilishwa ndani ya bunge la shirikisho. Fanya bunge la shirikisho lipitishe sheria yakuanzisha tume lakitaifa lawa Aboriginal linalo aminika, tume hilo linaweza weka vipaumbele kwa usambaaji wa rasilimali ili jamii zawa Aboriginal wawe na hali bora zaidi.”
"Pili, naweza omba bunge la shirikisho lipitishe muswada kwa tume ya mkataba na, tume hiyo ya mkataba inastahili chukua rasimu ya mkataba; nadhani ukiwa na vitu hivyo viwili, inaweza fanya tofauti halisi kwa maisha yawa Aboriginal," ali elezea zaidi.
Serikali ya shirikisho imeweka pamoja kundi tatu za ushauri, kuunda kwa pamoja, 'Sauti' kwa watu waki Aboriginal, wakifanya kazi katika ngazi za juu, kitaifa, kanda na mashinani.
Profesa Tom Calma ni mwanaume kutoka jamii yawa Kungarakan na Iwaidja, yeye ni mwenyekiti mwenza wa kundi la washauri la ubunifu wenza wa serikali ya shirikisho.

The red rock face of Uluru at sun set, the sacred home for thousands of years of the Yankunytjatjara and Pitjantjatjara people in the central Australian desert. Source: Getty Images AsiaPac
Ame elezea kuwa jukumu lao nikuwasilisha mifumo kadhaa kwa serikali ya shirikisho, ambayo ita amua muundo wa 'sauti' hiyo.
"Tuna taarifa ya tume za mkataba ila, zoezi letu halihusu kutazama mikataba. Ni wazi kuwa inahusu sauti kwa bunge."
Ripoti hiyo imekalishwa, mpango wa serikali ya shirikisho niku weka ripoti hiyo mbele ya baraza la mawaziri liizingatie, iitoe kwa mashauriano kisha watengeze sheria, yote hayo kabla ya uchaguzi ujao.
Kwa vikundi ambavyo havina nia yakufanya mwafaka kwa mifumo wanayo pendelea, Profesa Calma amesema watu waki Aboriginal wanastahili chukua faida ya fursa iliyo mbele yao.
"Nadhani tunacho stahili fanya nikutazama ya sasa, tunaweza fanikisha nini? nini kitafanikishwa bila kuathiri uadilifu wetu kama wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait?
“Tuna waziri mkuu unaye unga mkono waziri wa maswala yawatu wa asili, kutaka kuendeleza sauti kwa serikali na sauti kwa bune. Na kwa hiyo, tunastahili teka hilo na, tunastahili chukua faida ya hilo wakati tunaweza."
Maendeleo yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, yamepiganiwa, tangu wazungu walipo tua katika fukwe zawa Aboriginal.
Wakati wakuamua kati ya mifumo yakutambuliwa, jamii zawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, wamekubaliana kufikia kutambuliwa kwa maana katika wakati wa historia ya Australia, wakati serikali imeweka utambulisho na sauti kwenye ajenda ya taifa.