'Shughulikia pengo la mawasiliano': Jamii yawa Afrika ya Melbourne yaeleza serikali baada ya amri ngumu yakubaki ndani.

Katika sehemu ya pili ya makala yetu yaliyo rekodiwa,'Njia yakutoka katika Janga,' tunakuletea sauti za baadhi ya wakaaji wenye asili ya Afrika nchini Australia, kutoka minara ya makazi ya umma ya vitongoji vya Flemington na North Melbourne, ambao wamesema wamejifunza kutoka amri yakubaki ndani ya 2020.

Minara ya makazi ya umma mjini Melbourne, ilikabiliwa kwa amri kali yaku baki ndani katika mwezi wa July 2020.

Minara ya makazi ya umma mjini Melbourne, ilikabiliwa kwa amri kali yaku baki ndani katika mwezi wa July 2020. Source: David Crosling/AAP PHOTOS, Jul 2020

Wakaaji katika minara ya makazi ya umma katika kitongoji cha Flemington mjini Melbourne, wame kabiliana na masharti magumu zaidi ya vizuizi nchini tangu mwaka jana, wana kabiliana na milipuko ya maambukizi ya mwaka huu baada ya masomo waliyo jifunza.

Ilikuwa jibu gumu zaidi kwa mlipuko wa COVID-19, kutekelezwa nchini Australia kama vizuizi kwa uwezo wawatu kutembea nakujumuika bila onyo na, wakaaji hawaku ruhusiwa kutoka nje ya nyumba zao hata kwa sababu yakununua vitu mhimu kama chakula, madawa au kufanya mazoezi.


Mambo mhimu:

  • Jamii yawa Afrika ya Melbourne yasema ni vigumu kusahau amri ngumu za 2020 
  • Wakati masomo yamefunzwa, mengi zaidi yanahitajika kufanywa kushughulikia pengo la mawasiliano.
  • ‘Kushirikishwa kwa wafanyakazi wa jamii nama GP kutasaidia,' wanachama wa jamaii zawa Afrika wamesema


Serikali ya Victoria wakati huo ilikuwa imesema wakaaji walistahili fungiwa ndani kwa sababu, ya idadi ya kesi za coronavirus zilizo kuwa ndani ya majengo hayo.

Wakaaji wengi katika majengo hayo wanatoka katika mazingira ya pato dogo au jamii zawahamiaji, idadi kubwa ya watu kutoka Mashariki Afrika wakijumuishwa.

Mwaka mmoja baadae, kumbukumbu ya tukio hilo inaendelea kuwa hai ila, wakati Melbourne inapo kabiliana na wimbi lingine la mlipuko wa coronavirus pamoja na amri ya sita yakubaki ndani, je kuna chochote kilicho badilika kwa wakaaji wa minara ya makazi ya umma?

Public housing tower resident Barry Berih
Public housing tower resident Barry Berih. Source: SBS-Abby DInham

Pengo la mawasiliano ya COVID

Barry Berih, alizaliwa Australia kwa wazazi wenye asili ya Eritrea, alikuwa ndani ya nyumba Kaskazini Melbourne anayo changia na ndugu yake na mamake, wakati tangazo la amri yakubaki ndani lilipo tolewa mwaka jana.

Kuzingatia uzoefu huo, mtazamo wake ni upi kwa mlipuko wa sasa wa Melbourne na, utoaji wayo wa chanjo? Ni mafunzo yapi alijifunza?

"Uhaba wa mawasiliano," alisema, ilikuwa swala lililo zingira COVID wakati huo na linaendelea inapokuja kwa swala la chanjo.
Hakuna taarifa kutoka kwa GP wetu, kuwepo [kwetu] , kusema ni sawa ichukue au usi ichukue
Bw Berih na ndugu yake walitambuliwa baadae kuwa wana COVID-19, katika amri yakuto toka ya mwaka jana.

Ameomba rasilimali zaidi zipewe jamii, kuziwezesha kukabiliana na mlipuko wa sasa na utoaji wa chanjo. 

“Swali ni, ni rasilimali gani unaweza toa kwa jamii yawa Afrika, kwa watu wanao athiriwa na COVID-19, watu ambao wanajitenga kwa siku 14,” ali uliza.

Bw Berih, ambaye alipata COVID katika mtaa wa 33 Alfred Street, North Melbourne, alikuwa mtu mhimu waku andaa msaada kwa jamii kutokea ndani.
Nadhani, ajiri tu jamii zenye tamaduni tofauti kufanya kazi hii
"Wana elewa lugha na

[serikali inastahili]
toa rasilimali za ziada kwa watu wanao fanya kazi hiyo,” alidokeza.
Amharic  news 19 July, 2020
Bango katika moja ya mnara wa makazi katika barabara ya Racecourse, Flemington, Melbourne. Source: AAP

Pata msaada kutoka wafanyakazi wa jamii yawa Afrika

Bw Berih hayuko mwenyewe aki toa ombi la mahitaji yaku jumuisha watu wenye asili ya Afrika katika nguvu kazi inayo toa huduma kwa jamii yao.

Machot Achol nimu Australia aliye zaliwa Kusini Sudan, na anajiita "raia mwenye wasiwasi".

Amesema kuwajumuisha wanachama wa jamii yawa Afrika, kusaidia kutoa taarifa kunaweza kuwa na faida.

“Tunawatu wengi wanao fanya kazi katika hiyo sekta, inaweza kuwa wazo zuri kuleta baadhi yao ndani ili, watu wanapo waona, ita wahamasisha 

[kuchanjwa]
. Nadhani hiyo intakuwa hatua sahihi," Bw Achol ali ongezea.

Nataka wachangie taarifa na wanachama wa jamii na viongozi kwa sababu unapo fanya hivyo, [kupitia] vyanzo vya mawasiliano na jamii, itakuwa rahisi.
Bw Achol ame hamasisha pia pawe maboresho madogo kwa mawasiliano ya serikali na jamii yawa Afrika, kwa COVID na utoaji wa chanjo ila, angependa kuona mengi yakifanywa.

Katika taarifa, Idara ya Afya ya Victoria imesema kuwa huwa ina wasiliana na wakaaji kupitia mitandao mbali mbali kabla vizuizi vyovyote viwekwe.

“Mawasiliano huundwa kuambatana na jamii katika kila makazi na inajumuisha kuweka matangazo ndani ya visanduku vya barua, kubisha mlangoni pamoja nakutuma ujumbe moja kwa moja. Matukio yanayo kutanisha watu yalifanywa pia kabla ya vizuizi vya afya kuanza kutumiwa,” msemaji wa idara hiyo aliambia SBS Somali.

Hamdi Ali
Mkaaji wa makazi ya Carlton, Hamdi Ali Source: provided by the talent

Huduma zilizo boreshwa, mengi yanahitajika

Hamdi Ali, ana ishi katika minara ya makazi ya umma ya Carlton, alikuwa sehemu mhimu yakuratibu shughuli zakusaidia wakaaji wakati wa amri yakubaki ndani.

Naye pia amesema bado kuna pengo la mawasiliano, kati ya wakaaji na mamlaka.
Kwa bahati mbaya, si amini chochote kime badilika
Ila amekiri kuwa baadhi ya huduma zime boreka, kuna mashirika mapya yanayo wasaidia wakaaji.

“Kuna shirika lenye jukumu lakuwasaidia wakaaji katika minara ya North Melbourne na Flemington katika uponaji wa kiwewe cha amri yakubaki ndani,” aliongezea.

Majibu mengine kwa usambaaji wa virusi, yame boreka pia yakijumuisha utekelezaji wa mpango mpya wa chanjo na mlipuko mpya, na vipaumbele vimetolewa kwa wakazi.

“Wakaaji hawaku gawanywa katika vikundi vya miaka. Wakaaji wote wa makazi ya umma kuanzia miaka 16 na zaidi, kama wangeweza thibitisha wana ishi ndani ya minara ya makazi ya umma, wali stahiki.

[kupata chanjo]
,” Bw Ali alisema.

 

Ustahiki rahisi kwa chanjo

Geuzi kubwa kati ya mwaka jana na mwaka huu ni jinsi serikali ya jimbo, ime simamia mlipuko katika minara hii ya makazi ya umma kwa uwepo wa timu za chanjo.

Katika taarifa, Idara ya afya ya Victoria ilitangaza ustahiki wa wakaaji hao kwa chanjo ya Pfizer.

“Wanao ishi au kufanya kazi katika makazi ya hatari, wame stahiki kupokea chanjo ya Pfizer bila kujali umri wao tangu Julai 2021 na wamekuwa na uwezo waku hudumiwa kwa miadi iliyo hifadhiwa katika zahanati za chanjo zinazo simamiwa na serikali ya jimbo,” taarifa hiyo ilisema.

Serikali yatoa pendekezo la uhamisho

Serikali ya jimbo hilo ilitoa pendekezo kwa baadhi ya familia zenye watu wengi ambazo, zina ishi katika nyumba za umma ambazo hazi wafai, walipewa uamuzi wakuhamia katika makazi binafsi katika sehemu za nje ya mji.

Inakadiriwa takriban idadi ya familia 100 zilikubali pendekezo hilo.

Miongozi mwa familia hizo ni familia ya Abdirahman Magan, ambayo ilihama kutoka minara ya makazi ya umma, nakuingia katika nyumba katika moja ya vitongoji vya kaskazini Melbourne.

Miongoni mwa changamoto alizo simulia kulikuwa; kusomea mtandaoni ndani ya nyumba ndogo ambayo imejaa watu, hiyo ilikuwa changamoto.

“Pengine nyumba inawatu wengi. Ni vigumu kwa watoto ku keti waki karibiana wakati wanasikiza masomo au wanazungumza na walimu ila, nyumba hii inasehemu nyuma ya nyumba na, sehemu tofauti ambako watoto wanaweza keti na kompyuta zao, hiyo ni tofauti kubwa,” alisema.

Bw Magan amehamasisha familia zingine, zichukue fursa hii na zihame.
Ni bora kwa familia kuhamia ndani ya nyumba za chini
Mabadiliko ya mpango au moyo?

Hamse Isse ni mkaaji ndani ya moja ya minara hiyo, na ana uzoefu wa amri kali yangu baki ndani ya mwaka jana.

Anaona mabadiliko makubwa kwa jinsi minara hiyo ina simamiwa kwa sasa, katika mlipuko wa sasa wa Melbourne.He sees a big improvement in the ways the towers are now managed during Melbourne’s current outbreak.
Kama kesi za COVID zinatambuliwa katika Kiwango cha 3 au Kiwango cha 1 [cha mnara] , ni kwango hicho tu kitakacho tengwa na kila mtu humo ata ombwa aingie katika karantini ndani ya nyumba zao, au watapelekwa sehemu nyingine kwa siku 14
Victorian health officials work to conduct testing during a lockdown of a Melbourne public housing tower.
Victorian health officials work to conduct testing during a lockdown of a Melbourne public housing tower. Source: AAP

Ana amini chanjo ndani ya minara hii inaendelea kwa kiwango kizuri ila anakiri baadhi ya watu, wanahitaji kushawishiwa zaidi. Bw Abdisamad alitoa mchango wake pia kuongeza viwango vya chanjo.

“Chakushangaza nikwamba siku niliyo chanjwa, ilinibidi niwashawishi rafiki zangu sita waje nami katika kituo cha chanjo kwa kuwaelezea, ‘tuongezeni kiwango cha chanjo’, Bw Abdisamad alieleza SBS Somali.

Nia sahihi, mazoezi mabaya

Deborah Glass ndiye Mchunguzi wa malalamishi jimboni Victoria, baadae alipata kuwa wakati amri yakubaki ndani ili tetewa kwa misingi ya afya ya umma, utekelezaji wake wa mara moja haukuwa sahihi.

Alipendekeza pia serikali ya jimbo iwaombe msamaha wakaaji wa minara ya makazi ya umma, si kwa amri yakubaki ndani ila, kwa utekelezaji wa amri hiyo pamoja na kukiuka haki za binadam.

Makala haya yame andaliwa kwa ushirikiano na; SBS Tigrinya, SBS Dinka, SBS Swahili na SBS Amharic.


Share
Published 9 October 2021 3:21pm
By Hassan Jama
Presented by Gode Migerano
Source: SBS Somali


Share this with family and friends