Waaustralia walikabiliwa na sherehe za Mwaka Mpya mwaka huu, ambazo ziligubikwa na vizuizi vya janga la virusi vya corona vilivyowekwa kote nchini.
Matukio mengi ya fataki yalihairishwa, vikwazo kwa wageni katika kaya viliwekwa na watu waliambiwa wasibusu au kukumbatia wengine wanaposherehekea mwisho wa mwaka ambao ulikuwa wa kutisha kwa wengi.
Ukiwa na vizuizi vingi, hapa utaweza kusoma jinsi miongozo ya kile ulichoweza na usichoweza kufanya wakati wa mwaka mpya.
New South Wales

Source: SBS News
Isipokuwa ni wale ambao ni wakazi wa ukanda wa Kijani, watu walio na maombi ya awali ya kukutana katika mgahawa au wafanyakazi.
'Eneo la Njano' pia lilianzishwa karibu na Ukanda wa Kijani.
Kuingia kwa eneo la Njano hakukuzuiliwa kwa wakazi au wageni, lakini watu waliokusanyika katika maeneo haya kwa idadi kubwa waliweza kuhamishwa na polisi, Afya NSW walisema.
Ilikuwa kwamba ikiwa unakaa Greater Sydney (ambayo inajumuisha Wollongong, Central Coast na Blue Mountains) uliruhusiwa tu kuwa na wageni watano, pamoja na watoto, nyumbani kwako.
Pia uliruhusiwa watu 30 kwa mikusanyiko ya nje, ikiwa ni kiasi kidogo kutoka 50 kwa idadi iliyopita.
Wakazi wanaoishi katika ukanda wa kaskazini mwa Fukwe za Kaskazini walibaki chini ya maagizo makali ya kukaa nyumbani hadi angalau Januari 9, hata hivyo wakazi walipata msamaha kwa Mwaka Mpya ambapo iliwaruhusu kukaa hadi watu watano, pamoja na watoto, katika nyumbani kutoka mkoa huo huo.
Wale walio katika ukanda wa kusini wa Fukwe za Kaskazini pia waliruhusiwa kukaa hadi watu watano, pamoja na watoto, nyumbani kwao, pia kutoka ukanda huo huo, lakini hawakuruhusiwa wageni kutoka Greater Sydney.
Baa, migahawa na kumbi katika maeneo yote mawili ya Fukwe za Kaskazini ilibaki wazi kwa kuchukua chakula na vinywaji tu.
Nje ya Sydney, watu walishauriwa kuwasiliana na baraza lao ili waone kile wamepanga na ni vizuizi na miongozo gani iliyowekwa.
Queensland
Fataki kuu za Brisbane zilihairishwa, na kubusu na kukumbatia wageni pia kulishauriwa kutofanyika.
"Sisi sote tunapenda Mkesha wa Mwaka Mpya kumpa busu au kumbusu mtu wa karibu zaidi, ningependekeza upunguze hilo kwa marafiki wako wa karibu na familia," afisa mkuu wa afya wa serikali Dkt Jeannette Young alikaririwa akisema mapema kabla ya mkesha wa mwaka mpya.
Kaya ziliweza kuwa na wageni hadi 50, pamoja na wenyeji wa nyumba hiyo.
Mikusanyiko ya nje ya hadi watu 100 pia iliruhusiwa.
Victoria
Kuanzia saa kumi jioni katika siku ya mkesha, Wa-Victoria walilazimika kuvaa barakoa ndani ya nyumba ikiwa wako nje ya nyumba zao.
Wa-Victoria pia waliruhusiwa wageni 15 nyumbani mwao na mipaka ya kukusanyika katika kaya ikiwa nusu kutoka watu 30.
Wakazi wa Victoria huko Wollongong au Blue Mountains ambao walisafiri kutoka 27 Desemba waliweza kulazimika kufuta mipango yao ya mwaka mpya kabisa na walitakiwa hadi 11.59pm usiku wa mkesha kurudi Victoria.
Wasafiri pia waliomba kibali kipya cha kusafiri kurudi, kupimwa ndani ya masaa 24 na kujitenga nyumbani kwa siku 14.
Maonyesho ya fataki ya kila mwaka ya Melbourne juu ya Mto Yarra yalifutwa na serikali ya jimbo iliwataka watu kukaa mbali na maeneo ya mjini (CBD) ya Melbourne, ikisema kwamba ni wale tu walio na nafasi kwenye ukumbi jijini wataruhusiwa kuingia.
Baa, migahawa na kumbi zingine kama vilabu vya usiku vilikuwa wazi, lakini kwa idadi fulani ya wateja.
Australia Magharibi
Kulikuwa na maonyesho kadhaa ya fataki kote katika jimbo kuanzia saa 2 usiku na kuendelea - orodha kamili iliweza kutazamwa hapa.
Jimbo halikuwa na kiwango cha juu cha idadi ya watu walioruhusiwa kukusanyika, ikiwa hakuna zaidi ya mtu mmoja kwa kila mita mbili za mraba.
Australia Kusini
Fataki zilifutwa huko Adelaide lakini bado zilifanyika katika halmashauri za mitaa za Murray Bridge, Whyalla, Victor Harbor na Port Lincoln.
Mikusanyiko ya kaya ya hadi watu 50 iliruhusiwa, ikiwa hakuna zaidi ya mtu mmoja kwa kila mita mbili za mraba.
Hadi watu 200 waliweza kukusanyika kwenye ukumbi kwa shughuli za kibinafsi, ikiwa walitii sheria sawa ya mita za mraba.
Wakazi wa NSW pia walifungiwa kuingia Australia Kusini kuanzia usiku wa manane siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu wa Australia Kusini Steven Marshall alitangaza.
Kulikuwa na eneo la katazo la kilometa 100 kwa jamii zinazovuka mpaka na baadhi ya tofauti zilikuwepo kwa wakazi waliorudi, wale waliohama kabisa au wasafiri muhimu.
Hata hivyo, bado walihitajika kukaa siku 14 za karantini.
Tasmania
Hobart ilisherehekea mwaka mpya kwa sherehe zote za fataki za saa mbili na nusu huko River Derwent. Mwaka huu, hata hivyo, fataki zilionyeshwa juu sana kuliko kawaida kwa kuwa zilionekana kwa upeo wa wengi zaidi.
Tasmania ilikuwa na sheria ya mita mbili za mraba, lakini ikiwa na kikomo cha juu cha watu 250 kwa nafasi isiyogawanyika katika majengo ya ndani.
Nje, watu 1,000 waliruhusiwa kukusanyika katika eneo au majengo.

Hobart City fireworks Source: Hobart City Council
Jimbo la Mji Mkuu
Hakukuwa na maonyesho ya fataki mwaka huu katika mji mkuu wa Australia kwa mwaka wa pili mfululizo (mwaka jana walifuta kwa sababu ya mioto ya misitu).
Badala yake, wakazi walihimizwa kusherehekea kwenye migahawa ya vitongoji vyao na maonyesho ya taa za sherehe kwenye kumbi tofauti.
ACT haikuwa na vizuizi vyovyote kwa idadi ya wageni ambao watu waliweza kuwa nao katika nyumba zao.
Mikusanyiko ya nje katika mji mkuu Canberra ilipunguzwa kwa kiwango cha juu cha watu 500, ambapo sheria ya mita mbili za mraba iliweza kuzingatiwa
Jimbo la Kaskazini
Hakukuwa na mipaka kuhusiana na watu wangapi waliweza kukusanyika ndani ya nyumba au nje katika eneo la Kaskazini, lakini bado walishauriwa watu wakae mita 1.5 kutoka kwa watu ambao hawaishi nao wakati wote.