Baraza la mawaziri la taifa limeunga mkono hatua mpya za usafiri wa kimataifa na ndani ya nchi, kuimarisha ulinzi wa COVID-19, katika muitikio wa ongezeko la tisho la aina mpya ya mambukizi ya virusi vya corona kutoka Uingereza.
Sehemu kubwa ya Brisbane imetajwa kuwa eneo la hatari la virusi vya corona kwa kiwango cha madola baada ya, mfanyaji usafi kupatwa na aina mpya ya virusi vya corona, hali ambayo imefanya mji huo kufungwa kwa siku tatu.
Chini ya mageuzi hayo, wasafiri wanaowasili nchini Australia lazima wapatwe hawana COVID-19 baada yakupimwa, kabla yakuondoka mjini humo, pamoja na kupunguzwa kwa idadi ya wasafiri wanao rejea nchini.
Wasafiri katika ndege zinazotoka Uingereza, nao pia watafanyiwa vipimo kwa aina mpya ya virusi vya corona kabla hawajapanda ndege za kwenda kwao.
Itakuwa lazima kwa abiria wote katika ndege zinazo safiri ndani ya nchi na kimataifa kuvaa barakoa, pamoja na katika viwanja vya ndege nchini. Watoto wenye umri chini ya miaka 12 watapewa msamaha wa amri hiyo ndani ya viwanja vya ndege.
"Virusi hivi vinaendelea kuandika sheria zake zenyewe, na hiyo inamaana tunastahili kuendelea kubadili jinsi tunavyopambana navyo," Bw Morrison alisema.
Kutakuwa na misamaha kwa masharti ya upimaji, kama wafanyakazi wa misimu kutoka nchi zenye athari ndogo, ambako hakuna vipimo vingi, ambao badala yake watafanyiwa uchunguzi wa kipekee.
Idadi yawasafiri wa kimataifa wanaowasili nchini yapunguzwa hadi Februari
Idadi ya wasafiri wa kimataifa wanaowasili nchini Australia, imepunguzwa kwa asilimia 50 katika majimbo ya New South Wales, Magharibi Australia na Queensland.
Idadi ya wasafiri ambayo imefanyiwa tathmini jimboni New South Wales itapunguzwa hadi watu 1,505 kila wiki, idadi hiyo Magharibi Australia ni watu 512 kwa wiki na jimboni Queensland idadi hiyo imepunguzwa hadi watu 500 kwa wiki.
Jimbo la Victoria litaendelea kuwapokea wasafiri 490 kila wiki, baada ya idadi hiyo kupunguzwa kabla baada ya jimbo hilo kukabiliwa kwa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.
Baraza la mawaziri la kitaifa, liliafiki kupunguza idadi ya wasafiri wanaowasili hadi tarehe 15 Februari, katika kikao cha viongozi wa majimbo na mikoa hapo Ijumaa.
Bw Morrison ameongezea kuwa, asilimia 80 ya Waustralia waliosajiliwa ng'ambo, kwa sasa wako katika nchi ambako imethibitishwa aina mpya ya virusi hivyo ipo.
"Kuna mengi yasiyojulikana na hali ya kutokuwa na uhakika kwa upande wa aina hii mpya ya virusi na, ndiyo sababu tuna amini mbinu hii ya tadhari, ni busara sana," alisema.
Naye Afisa mkuu wa matibabu Paul Kelly amesema majibu ya haraka na imara, yalilenga kudhibiti athari za aina mpya ya maambukizi ya virusi vya corona.
"Swala letu kubwa ni kuhakikisha usalama wa Waustralia na kuhakikisha kuwa, aina hii mpya ya virusi haianzi kusambaa nchini Australia," alisema.
"Ni kwasababu itakuwa vigumu zaidi kuidhibiti."
Wafanyakazi wote katika sehemu za karantini, kwa sasa lazima nao pia wafanyiwe vipimo kila siku.
Wafanyakazi wa ndege za kimataifa nao pia lazima wafanyiwe vipimo vya COVID-19 nchini Australia kila baada ya siku saba au, wanapowasili na watahitajika kuingia katika karantini katika sehemu maalum katikati ya safari.
Takriban idadi ya watu elfu 38,000 wamesajiliwa na idara ya maswala ya kigeni na biashara, wakiwa wanataka kurejea nchini kutoka ng'ambo.