Sauti kwa bunge ni nini?
Katika mwaka wa, kundi la wawakilishi lawatu wa jamii yakwanza ya Australia, walijumuika Uluru, nakuwapa wa Australia hati iliyo pewa jina la .
Taarifa ya Uluru inapendekeza mambo matatu ya msingi ya mageuzi: Sauti, Makarrata (neno katika lugha yaki Yolngu linalo maanisha ) na
Mambo mhimu:
- Sauti kwa Bunge ni ombi la kuundwa kwa tume ya ushauri ya watu wa asili, kuongoza bunge ya shirikisho kwa maswala yanayo husiana na Watu wa Jamii ya Kwanza.
- Kauli ya Uluru kutoka Moyoni, inaomba mageuzi matatu mhimu ambapo Sauti kwa Bunge ni ya kwanza.
- Waandishi wa Kauli ya Uluru, wamependekeza Mei 2023 au Januari 2024 kuwa tarehe za kura hiyo ya maoni kufanywa.
Geuzi la kwanza ni Sauti kwa Bunge, ambayo ina hitaji mageuzi kwa Katiba.
Hiyo ina maan, inahitaji kura ya maoni ili, pendekezo hilo litolewe kwa wa Australia walifanyie maamuzi.
Ni mchanganyiko wa mchakato ulio dumu kwa miongo, ya mfumo wakisheria nakisiasa wa Australia na watu wa Australia wakiufanyia kazi kuelekea kutambuliwa katika katiba kwa jamii yawatu wa kwanza nchini.
Ina maana gani kwa wa Australia?
Kura ya maoni inaweza wauliza wa Australia, waidhinishe hatua mpya inayo ruhusu bunge la shirikisho, kuunda kundi la ushauri ambalo litajulikana kama Sauti kwa bunge.
Katiba ya Australia, ambayo ilianza tumika 1 Januari 1901, haiwatambui watu wa jamii zawa Aboriginal au Torres Strait Islanders kabla ya ukoloni na umiliki wa nchi.
Kimsingi, Sauti kwa Bunge ni kutambuliwa kwa jamii hizi za kale ambazo zime ishi katika bara hili kwa miaka elfu sitini, sauti zao na nafasi yao katika demokrasia ya Australia kupitia katiba ya Australia.
Profesa Megan Jane Davis ni mwenyikiti mwenza wa Mjadala wa Uluru, yeye pia ni mwanasheria haki zabinadam wakimataifa kutoka chuo cha New South Wales. Amesema inahusu pia kutambua watu wa Australia na bara kama “udhihirisho kamili wa taifa,” nakuruhusu nchi “iendelee mbele kwa mara ya kwanza katika historia yake.
“Ni sehemu ya idadi yamageuzi Kauli ya Uluru kutoka Moyoni imeomba, kwa upande wa mageuzi yanayo hitajika kuwawezesha watu wetu na hiyo inajumuisha Tume ya Makarrata, ambayo ni makubaliano yakutengeza au tume ya mkataba,” alisema.
“Kutambua sauti ya Jamii za Kwanza, kunawezesha watu wetu wawe mezani wakati sheria na sera zina tungwa kuhusu maisha yetu.”
Tuko wapi?
Baada ya hotuba yake yakukiri nchi, alianza hotuba yake ya ushindi usiku wa uchaguzi mkuu kwa kusema, “kwa niaba ya chama cha Labor cha Australia, najitolea kwa Kauli ya Uluru Kutoka Moyoni kwa ukamilifu.”
Katika kauli hiyo, Prof Davis amesema, “ni hisia ya afueni na mafanikio ila bado kuna safari ndefu”.
“Tumesisimka, ni nadra kwa Australia kubadili katiba yake. Na watu wetu, hatujawahi kuwa na fursa ya mamlaka yoyote kikatiba. Kwa hiyo, hiki ni kitu mhimu sana. Ni tofauti na kura ya maoni ya 1967, kwa sababu mageuzi haya yata wawezesha watu wetu,” aliongezea.
Kwa upande wa tamko la Uluru, sasa kuna ahadi kwa ajili ya kura ya maoni, ambayo ni hatua ya kwanza ya kauli hiyo na, serikali mpya ya shirikisho ina andaa namna yakufanya hivyo.
Hatua zinazo fuata
Kuna hatua mhimu kabla Sauti ya watu wa Asili, inaweza wekwa katika katiba.
Kulindwa kikatiba, Sauti itakuwa endelevu na itadumu, zaidi ya ratiba zakisiasa.
Ina maana kuwa uwezeshaji wa watu wa Asili na, ushiriki wao katika maisha yakidemokrasia ya taifa, havitegemei chama chakisiasa kitakacho kuwa madarakani.
Serikali ya awali ya mseto ilikuwa na nia yakuweka Sauti katika muswada ila, haikuwa na mipango yaku ijumuisha katika katiba na kama Sauti ingepitishwa katika sheria, inge weza batilishwa.
READ MORE

What does Welcome to Country mean?
Ila punde inapo wekwa ndani ya Katiba, inaweza batilishwa tu kupitia kura nyingine ya maoni. Hatua hiyo lazima ipata msaada wakisiasa na, majadiliano ya ziada kabla ya kura yoyote kupigwa.
Kama Bunge la sherikisho linapitisha Muswada, kura ya maoni lazima ifanywe ndani ya miezi sita kuunda kundi la ushauri lakudumu la jamii ya kwanza kwa bunge la shirikisho.
Waandishi wa Kauli ya Uluru wamependekeza Mei 2023 au Januari 2024 kama ambazo kura hiyo ya maoni inaweza fanywa.