Msako unaendelea kumtafuta msichana wa miaka tisa aliyetoweka kwa siku nne katika Milima ya Bluu ya NSW

Msako mkubwa umeanza tena katika Milima ya Bluu hapa NSW kumtafuta msichana mwenye umri wa miaka tisa Charlise Mutten, ambaye alionekana mara ya mwisho kwenye nyumba siku nne zilizopita.

A supplied image of nine-year-old Charlise Mutten who has been missing from a property at Mt Wilson, 60km north-west of Richmond, since Thursday.

A supplied image of nine-year-old Charlise Mutten who has been missing from a property at Mt Wilson, 60km north-west of Richmond, NSW since Thursday. Source: NSW Police

Msako wa kumtafuta Charlise Mutten mwenye umri wa miaka tisa umeanza tena baada ya msichana huyo wa NSW kutoweka siku nne zilizopita.

Wazazi wa Charlise wanasema walimwona msichana huyo mara ya mwisho siku ya Alhamisi katika eneo la Mlima Wilson, kilomita 20 kaskazini mwa Katoomba, NSW.

Aliripotiwa kutoweka siku ya Ijumaa, na kusababisha msako uliohusisha zaidi ya polisi mia moja na wafanyakazi wa dharura wakiwemo vitengo vya mbwa, helikopta za polisi na SES.

Charlise ni Caucasian, ana urefu wa kati ya 130cm na 140cm, na mwembamba. Ana nywele za kahawia na macho ya kahawia.

Inaaminika kuwa alikuwa amevalia nguo ya juu ya waridi yenye kola ya shingo ya mviringo, sketi nyeusi inayofikia goti na kandambili za rangi ya pinki za Nike.
Utafutaji wa mashirika mengi umetumia ujumbe wa kulenga kijiografia katika eneo la Mlima Wilson.
"Ingawa polisi wana wasiwasi mkubwa juu ya usalama wake, tunashukuru hali ya hewa imekuwa nzuri kwetu katika siku chache zilizopita na tunaamini hali ya hewa ingemtosha kuweza kuishi wakati huu msituni," Inspekta Mkuu Garry Sims alisema Jumapili. "Kuna maji msituni kwa hivyo tunatumai Charlise ataweza kujikimu hadi tutakapompata."

Share
Published 17 January 2022 4:46pm
Updated 17 January 2022 4:54pm
By Frank Mtao
Source: AAP, SBS


Share this with family and friends