Wa Australia wawili wazee wamefariki baada yakukabiliana na coronavirus, mmoja wao ni mkaazi wa hifadhi ya wazee ya Newmarch House mjini Sydney, pamoja na mwanamke mwenye umri wa miaka 86 aliye fariki katika hospitali ya Mersey Community ambayo iko katika eneo la kaskazini magharibi ya Tasmania.
Idadi ya vifo nchini kupitia coronavirus kwa sasa ni 93.
Hapakuwa taarifa nyingi kuhusu mkaazi huyo wa hifadhi ambayo iko karibu ya mji wa Penrith jimboni NSW, ambako kufikia sasa wazee 13 wamefariki kupitia kirusi hicho.
Shirika la Anglicare ndilo mmiliki wa hifadhi hiyo, shirika hilo lilichapisha taarifa ijumaa likisema limehuzunishwa na kifo hicho siku ya alhamisi na, shirika hilo limetuma risala za rambi rambi kwa familia husika.
Taarifa hiyo ilisema: "Coronavirus imekuwa na athari mbaya kwa wakazi wetu wote pamoja na familia na wafanyakazi wetu katika wiki tatu zilizo pita."
Alhamisi 30 Aprili 2020, wakaazi wengine watatu wa Newmarch, walitambuliwa kuwa wana virusi vya coronavirus.
Na takriban wafanyakazi 60 pamoja na wakazi katika hifadhi hiyo, pia wamepatwa na virusi vya coronavirus tangu mlipuko wa virusi hivyo katika hifadhi hiyo tarehe 11 Aprili.
Shirika la Anglicare limesema visa vipya vimejiri licha "yakutekeleza utaratibu mkali, wakudhibiti uambukizi.".
"Visa hivi vipya vina ashiria uambukizi wakihistoria na, vina ambatana na vipimo vinavyo fanywa katika hifadhi ya Newmarch House.
Tutachunguza zaidi, jinsi hali hii ilitokea."
Taarifa hiyo iliongezea kuwa, hifadhi hiyo imefanikiwa kuwasiliana zaidi na familia, pamoja na mafanikio ya familia kuzungumza na jamaa dirishani.
Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian alikiri Ijumaa kuwa, pamekuwa maboresho kuhusu jinsi kifaa hicho kime kuwa kikiwasiliana na familia za wakaazi.

Louise Payne, who has a family member living at Anglicare's Newmarch House arrives with family and friends at the agedcare home in Kingswood, near Penrith, NSW. Source: AAP
"Tumeitisha hiyo kwa sababu, kinacho fanyika hapo hakifai," Bi Berejiklian alieleza shirika la habari la ABC.
Kiongozi huyo aliongezea kuwa, wamiliki wa hifadhi za wazee, "wanastahili visimamia bora zaidi", kuhakikisha familia zawakaazi wanaweza watembelea.
"Jamaa yawakazi, hawastahili zuiwa, kuwatembelea wapendwa wao," alisema.
"Tunajua hadi tiba inapatikana, sote lazima tubadili jinsi tunavyo ishi nawasio jiweza hawastahili zuiwa kuwaona jamaa wao, kwa muda mrefu."
Mkusanyiko jimboni Tasmania
Jimboni Tasmania, kati ya vifo 12 kwa vifo 13 vya COVID-19 vimekuwa katika eneo la kaskazini magharibi na theluthi mbili ya jumla ya visa 221 ambavyo vime ungwa na mkusanyiko wa maambukizi, ambao una aminiwa yali anzia katika meli ya Ruby Princess.
Kifo chakipekee kusini mwa jimbo hilo, nacho kilihusishwa na msafiri wa meli ya Ruby Princess, ambaye alifia ndani ya hospitali ya Royal Hobart Hospital.
Ripoti ya mpito iliyo chapishwa Alhamisi, ilipata kuwa kiini cha mkusanyiko wa virusi ilikuwa wazee wawili ambao walikuwa wasafiri katika meli ya Ruby Princess, walio pokea matibabu katika hospitali hiyo mwisho wa mwezi Machi nawakafa baadae.
Takriban vifo 21 nchini ambavyo vimesababishwa na virusi hivyo, tayari vimeungwa na meli hiyo baada ya wafariri, kuruhusiwa kushukia mjini Sydney mwezi machi, kabla ya matokeo ya vipimo vyao kujulikana.
Mfanyakazi wa kwanza wa huduma ya afya katika eneo la Kaskazini magharibi, alipatwa na virusi vya corona tarehe 3 Aprili. Kufikia tarehe 21 Aprili, watu sabini na tatu walikuwa wame ambukizwa.
Alhamisi kiongozi wa Tasmania Peter Gutwein, aliwahamasisha watu wasiwalaumu wafanyakazi wa afya au abiria wa meli hiyo.
"Kimsingi hiki ni kisa cha watu wanao endelea na maisha yao, wanafanya kazi zao," alisema, akizungumza kuhusu meli ya Ruby Princess kama "chanzo".
Visa vingine viwili vilithibitishwa usiku wa alhamisi, kisa kimoja kikiwa katika eneo la kaskazini magharibi na kingine katika eneo la kaskazini.
Watu nchini Australia wanastahili kujipa mita 1.5 mbali ya watu wengine. Tazama vizuizi vya jimbo lako, kuhusu masharti yakujumuika.
Vipimo vya coronavirus kwa sasa vinaweza patikana kote nchini Australia. Iwapo unahisi dalili za mafua, unaweza pimwa kwaku mpigia daktari wako au kuwasiliana na namba ya taarifa ya afya kuhusu Coronavirus 1800 020 080.
App ya serikali ya shirikisho yaufuatiliaji kwa jina la COVIDSafe, inaweza pakuliwa kutoka duka la app ya simu yako.
SBS ime ahadi kutoa taarifa kwa jamii mbali mbali nchini Australia, kuhusu maendeleo mapya ya COVID-19. Unaweza pata taarifa na maelezo ya ziada katika lugha 63 kwenye tovuti hii