Hatua zifuatazo zili anza kutekelezwa kuanzia mchana wa tarehe 6 Mei 2021. Hatua hizo zitadumu hadi usiku wamanane wa Jumatatu tarehe 10 Mei, kwa maeneo ya kanda ya Sydney maeneo hayo yatajumuisha (Wollongong, Central Coast na Blue Mountains):
Idadi yawageni wanao ruhusiwa ndani ya nyumba ni 20, watoto wakijumuishwa.
Barakoa lazima zivaliwa ndani ya usafiri wa umma na ndani ya sehemu zote za umma, kama madukani, sehemu za burudani, hospitalini, vifaa vya huduma yawazee na, kwa wafanyakazi katika migahawa (isipokuwa ndani ya migahawa ambako wakati watu wanakula au wana kunywa.)
Watu hawata ruhusiwa kutumia vinywaji wakiwa wamesimama ndani ya sehemu za ndani zama tukio.
Ni marufuku kwa watu kuimba wakiwa ndani ya vyumba vya tamasha, au waumuni kuimba wakiwa ndani ya sehemu za ibada.
Ni marufuku kwa watu kucheza ndani ya sehemu za ndani za matukio au ndani ya vilabu vya burudani, hata hivyo, wanao hudhuria harusi wanaruhusiwa kucheza mziki lakini ni watu 20 tu watakao ruhusiwa kucheza kwa wakati mmoja.
Ni watu wawili tu ndiwo wataruhusiwa kutembelea makazi ya huduma ya wazee.
Kiongozi wa New South Wales Gladys Berejiklian amesema, vizuizi hivyo vitasaidia kupunguza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo.