Je! Rais Magufuli anapokea matibabu ya Coronavirus Kenya?

Tarifa zimetufikia kuwa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, anapokea matibabu nchini Kenya, baada yakupatwa na Coronavirus.

Rais Magufuli atao hotuba

Rais Magufuli atao hotuba Source: Ikulu Tanzania

Serikali ya Kenya na serikali ya Tanzania hazija thibitisha kama Rais Magufuli yuko nchini Kenya akipokea matibabu hayo.

Hata hivyo, mashirika kadhaa ya habari nchini Kenya yameripoti kuwa kiongozi mmoja wa taifa barani Afrika yuko ndani ya hospitali ya Nairobi, ambako anapokea matibabu ya Coronavirus. Mmoja wa viongozi wa upinzani kutoka Tanzania Tundu Lisu, ame eleza vyombo vya habari kuwa kiongozi huyo ambaye anapokea matibabu hayo ndani ya hospitali ya Nairobi, ni Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania.

Rais Magufuli alionekana mara ya mwisho hadharini, tarehe 27 Februari mjini Dar es Salaam katika tukio rasmi. Katika moja ya hotuba zake za hivi karibuni, Rais Magufuli aliwahamasisha watanzania, waepuke kutumia barakoa zinazo uzwa madukani kutoka ng'ambo, na badala yake wajishonee barakoa zao binafsi, ambazo alisema ni salama zaidi. Idhaa ya Kiswahili ya SBS, imeomba serikali husika taarifa rasmi kuhusu swala hili, na tuta kuarifu mengi zaidi, punde tutakapo pokea jibu rasmi.

 

 


Share

Published

Updated

By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS Swahili

Share this with family and friends