Je! Gharama ya makatazo ya COVID-19 kwa biashara ndogo na jamii ni gani?

Tangazo la serikali ya New South Wales kuongeza muda wa makatazo ya COVID-19 kwa wiki nne zaidi, lime waacha wamiliki wa biashara ndogo katika maeneo husika pabaya kifedha.

Biashara ndogo zimefungwa wakati wa makatazo ya COVID-19

Biashara ndogo zimefungwa wakati wa makatazo ya COVID-19 katika maeneo ya Greater Sydney Source: Pexels

 

Wamiliki wa biashara ndogo katika maeneo ya Greater Sydney, wanaendelea kukabiliana na madhara ya makatazo ya COVID-19.

Mabanda ya mighahawa nje ya soko kubwa katika kitongoji cha Liverpool, yaendelea kuwa matupu wakati wa makatazo ya COVID-19
Mabanda ya mighahawa nje ya soko kubwa katika kitongoji cha Liverpool, yaendelea kuwa matupu wakati wa makatazo ya COVID-19 Source: AAP

Wengi wao hawaja weza fanya biashara yoyote tangu serikali ya jimbo hilo, ilipotangaza kusitishwa kwa biashara zote katika sehemu ya makatazo yakukabiliana na usambaaji wa virusi vya COVID-19 ndani ya jamii.

Bi Nava ni mmoja wa wajasiriamali ambao biashara yake ime athiriwa na amri ya makatazo hayo, katika mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, ali elezea wasiwasi wake kwa ustawi wa biashara yake pamoja na wafanyakazi wake, wengi ambao hakuwa na budi kuwasimamisha kazi kwa sababu ya makatazo hayo.

Wakati huo huo mamlaka jimboni NSW, wameongeza idadi ya zahanati ambako wakaaji wamaeneo husika wanaweza fanya vipimo vya COVID-19, hususan kwa wanao hitaji vipimo hivyo ili waendelee kufanya kazi.

COVID TEST CLINIC FAIRFIELD SHOWGROUND NSW
Magari yapiga foleni katika kituo cha vipimo vya covid-19 katika kitongoji cha Fairfield, NSW Source: AAP Image/Mick Tsikas

Na katika jimbo la Kusini Australia, Deborah Kalei ndiye kiongozi wa chama cha KASA, ambacho huwakilisha nakutoa huduma kwa wakenya jimboni humo. Katika mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bi Deborah aliweka wazi hatua ambazo viongozi wa chama chake, wame chukua kuwanusuru wanachama ambao wanakabiliwa na changamoto za COVID-19 jimboni humo.

Deborah Kalei, Rais wa KASA akiwa kwenye zulia jekundu
Deborah Kalei, Rais wa KASA akiwa kwenye zulia jekundu. Source: Deborah Kalei
Moja ya hatua ambazo uongozi wa Bi Deborah ulichukua, ilikuwa kushirikiana na maduka mawili mjini Adelaide, ambayo wanachama wa KASA wanao kabiliwa na matatizo yakifedha wakati wa makatazo na vizuizi vya COVID-19, wanaweza wasilisha hati maalum katika maduka husika nakupewa vyakula bila malipo yoyote.

Bi Deborah ali eleza Idhaa ya Kiswhaili pia, kuhusu changamoto ya baadhi ya wanajamii ambao wana endelea kusita, kupokea msaada licha yakuwa misaada hiyo inatolewa bure kwa anaye ihitaji.ya SBS kuwa, yeye pamoja na viongozi wenza wana mikakati yakuwasaidia wanachama watakao hitaji msaada kutoka kwa KASA.

 


Share

Published

By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS Swahili

Share this with family and friends