Usambaaji wa virusi vya coronavirus, umelazimisha viongozi katika majimbo ya New South Wales, Victoria na Queensland kuweka amri za makatazo na vizuizi mbali mbali, kwa ajili ya kuzuia uambukizaji wa virusi hivyo ndani ya jamii. Licha ya maamuzi hayo yenye lengo laku linda umma dhidi ya maambukizi ya coronavirus, maamuzi hayo yamepokewa kwa hisia mseto na baadhi ya wanachama katika jamii. Katika mazungumzo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, mkaaji wa Sydney Bi Nancy alisisitiza kuwa "ni vizuri kuzuia usambaaji wa virusi hivi kuliko kajaribu kutengeneza, wakati janga hili litakuwa sababisha uharibifu tayari."
Katika kanda ya Central Coast jimboni New South Wales, Bi Rahab alifunguka kuhusu masaibu yanayo wakumba watu wanao kabiliana na changamoto za afya ya akili hususan wakati huu wa makatazo ya COVID-19. Bi Rahab alieleza Idhaa ya Kiswahili kwamba, "tatizo kubwa ni uhaba wa huduma zinazo stahili kwa watu wenye ugonjwa wa akili, mara nyingi wanao tuhudumia hawa jui chakufanya na hawana uelewa wa ugonjwa wa akili. Kama unaishi mwenyewe pia ni tatizo maana, hauna wakuongea naye wala kutembelea kwa hiyo unahisi umelemewa."
Na mjini Wollongong wakaaji nao walipokea amri ya makato ya COVID-19 kwa hisia mseto, Pasi ni mkaaji wa Wollongong. Alipozungumza na idhaa ya Kiswahili ya SBS alisema: "Nahisi ni kama tuna adhibiwa kwa dhambi za watu wa Sydney. Wame shindwa kudhibiti ugonjwa huu, sasa sisi pia tuna adhibiwa." Licha ya kauli hiyo, Bw Pasi alikiri kuwa makatazo ya serikali yata saidia kudhibiti maambukizi ya virusi vya COVID-19 ndani ya jamii. Ali wahimiza wanachama wa jamii pia, waitikie mwito wa chanjo, sawa vile alivyo fanya yeye binafsi nakupoa chanjo zote mbili za COVID-19.
Ongezeko la visa vya maambukizi ya COVID=19 jimboni New South Wales na Victoria, vime sababisha mipaka kati yamajimbo hayo kufungwa na wasafiri lazima wawe, na vibali maalum kwa ajili yakupewa ruhusa yakutoka nakuingia.