Feature

Je sehemu za kazi nchini Australia zina stahili ondoa masharti ya chanjo ya UVIKO?

Makampuni kama na Qantas yamefuta masharti ya chanjo ya UVIKO-19 kwa wafanyakazi wao. Ila waajiri wengi wanaendelea kuwataka waajiriwa wao wawe wamepata chanjo zote, licha ya mamlaka zama jimbo na wilaya kusitisha amri za afya ya umma.

Female medical student raising hand in class

Experts say vaccines don't prevent COVID-19 transmission for a long period. (Representative image) Credit: Fly View Productions/Getty Images

Highlights:
  • NSW Premier Dominic Perrottet said COVID-19 vaccines don't stop transmission
  • Professor Peter Collignon said vaccine mandates should be scrapped
  • AMA President Steve Robson supports COVID-19 vaccine requirement for doctors
Laura (jina lake limebadilishwa) ni mfanyakazi wa zamani wa huduma ya afya, amesema alisimamishwa kazi bila malipo na hatimae miaka mbili iliyopita alifutwa kazi kwa kukataa kuchukua chanjo ya UVIKO-19 kwa sababu binafsi.

Laura, ambaye ndiye mfanyakazi pekee nyumbani kwake, ilibidi afanye kazi kadhaa, kuuza mali zake pamoja nakutumia hela alizo kuwa ameweka kwenye akiba kukidhi mahitaji ya familia yake.

"Siwezi mudu mafunzo yaku ogelea au miadi ya daktari wa watoto wangu. Amri hizo hazikustahili tolewa. Haya ni mapato ya mtu, si swala dogo," Laura alieleza SBS.

"Sasa kuna taarifa ya umma kuwa chanjo hazi kingi wala kuzuia maambukizi. Kwa hiyo ni kwa nini watu kama mimi wali adhibiwa sana kwa kitu ambacho kilikuwa hakija thibitishwa wakati huo.," aliuliza.
Mahojiano ya hivi karibuni ya kiongozi wa New South Wales Premier Dominic Perrottet, yame ibua tena mjadala kuhusu amri za chanjo za UVIKO-19.

"Hakuna ushahidi kuwa chanjo zina zuia maambukizi," Bw Perrottet ali eleza .

Je chanjo huzuia maambukizi?

Profesas Steve Robson, ni Rais wa shirika la Australian Medical Association, amesema si kweli kuwa chanjo hazi zuii maambukizi.

"Kama mtu ambaye ame chanjwa anapata UVIKO-19, wana uwezo mdogo waku waambukiza watu wengine kuliko kama hawaja chanjwa kabisa," Prof Robson alieleza SBS.

Prof Robson alichangia utafiti ulio chapishwa katika jarida la Nature tarehe 26 Agosti 2022 kama ushahidi kuwa chanjo ya UVIKO pamoja na maambukizi ya kabla, hupunguza hatari yaku sambaza virusi vya Omicron.

Ila, utafiti huo pia ulibaini kuwa " faida za chanjo kupunguza maambukizi ya Omicron hazi dumu kwa muda mrefu."
Coles
On 1 March 2023, Coles joined other Australian employers in dropping their COVID-19 vaccination requirement for its team members at stores, distribution centres and other sites. Source: AAP / JAMES GOURLEY/AAPIMAGE
Profesa Peter Collignon, ni daktari wa magonjwa yaku ambukiza pamoja nakuwa mwanabailojia katika hospitali ya Canberra, amesema chanjo hupunguza maambukizi.

"Ila si kwa wingi kama vile wengi wetu wange tarajia," Prof Collignon alisema.

"Hili ni swala haswa tangu aina ya virusi vya Delta na Omicron vilipo sambaa pamoja na uwezo wavyo waku kwepa madhara ya chanjo.
They (vaccine) still prevent about 30 per cent of mild infections but only for a few months
Professor Peter Collignon
Profesa Catherine Bennett, ni mwenyekiti wa idara inayo simamia maswala yakusambaza nakudhibiti magonjwa ambayo kwa lugha yakitaalam inajulikana kama epidemiology katika chuo cha Deakin, amesema hakuna tafiti zenye maelezo ya kina kuhusu maambukizi kwa chanjo mpya zinazo lenga aina mpya ya virusi.

"Ila tunajua ufanisi dhidi ya maambukizi ulipunguzwa kwa chanjo za kwanza wakati aina ya kirusi cha Delta kilipo ibuka," Profesa Bennett alisema.

"Data mpya kutoka Uingereza inaonesha kuna angalau ufanisi wa muda mfupi wa kati ya miezi mbili hadi mitatu, kwa kupunguza hatari ya maambukizi kufuatia kupewa chanjo ya jeki."

Je sehemu za kazi zinazo salia zinastahili sitisha amri za chanjo?

Baadhi yamakampuni binafsi, huduma za dharura, makaazi ya huduma ya wazee na walemavu pamoja na mashirika yanayo toa huduma ya afya, yana endelea kusisitiza kuwa wafanyakazi wao wawe wamepata chanjo zote, wakitaja sheria za afya yakazini na usalama.

At this stage, given the poor performance of vaccines in stopping or decreasing transmission, we should no longer have mandates
Prof Collignon
"Ni mhimu zaidi kuhakikisha wakaaji wote wa makaazi ya huduma yawazee wame chanjwa na wamepata chanjo za jeki. Hiyo ndiyo mbinu itakayo punguza vifo vya UVIKO," Prof Collignon alisema.

"Msisitizo kwa amri za chanjo kwa wafanyakazi wachanga si sahihi. Msisitizo unastahili kuwa kwa wazee, haswa wale ambao wamo ndani ya makaazi ya huduma yawazee," Prof Collignon aliongezea.
Hata hivyo Rais wa shirika la AMA Prof Robson, ana maoni tofauti.

Prof Robson amesema kuwa idara za afya za Australia, zimetoa amri za chanjo za mafua na Hepatitis B kwa wafanyakazi wa huduma ya afya ambao hugusana na wagonjwa pamoja na sampuli za vipimo vya wagonjwa hao.

"Hali hiyo huwalinda wagonjwa pamoja na wafanyakazi wa huduma ya afya katika sehemu za kazi," aliongezea.

"Wagonjwa wanao pokea huduma ya wazee na walemavu mara nyingi huwa wako katika hali tete sana. Kwa sababu hizo, tuna wasaidia madaktari wanao hudumia wagonjwa hao situ dhidi ya maambukizi ya UVIKO ila pia kwa magonjwa mengine yakuambukiza."
Prof Bennett amesema kila hali inastahili fanyiwa uchunguzi wa hatari ya maambukizi.

"Sehemu za kazi zenye kiwango cha juu cha maambukizi, zita hitaji kuwa na baadhi ya sheria zinazo stahili zinazo saidia kudhibiti hatari hiyo," alisema.

"Ni busara kuwa mazingira yenye hatari kubwa kama huduma ya afya, ambayo tayari yana masharti kuhusu chanjo za mafua, yanaweza kuwa na masharti sawia kwa UVIKO."

Msimamo wa serikali ni upi?

Idara ya Afya na Huduma ya Wazee ya Australia, imesema ina unga mkono chanjo, ila msimamo wa serikali kwa chanjo za UVIKO-19 ni kwambo nikwa kujitolea.

"Serikali ya Australia haiwajibiki kwa amri zozote za chanjo," idara hiyo ili eleza SBS kupitia taarifa iliyotuma.

"Amri ya umma zamajimbo na mikoa, zinaweza toa masharti ya lazima ya chanjo kwa baadhiya kazi pamoja na misamaha midogo ambayo inaweza tolewa," taarifa hiyo iliongeza.

Idara ya Afya ya NSW ilikataa kutoa taarifa, ikisema ni swala la serikali ya jimbo, wakati Idara ya Afya ya Victoria, ilisema ni wajibu wa sehemu za kazi binafsi, kuwa na sera zao binafsi kuhusu chanjo.

Kurejea kwa wafanyakazi wa huduma ya afya

Mfanyakazi wa Huduma ya afya Laura, "bado yuko kwenye njia panda kimawazo" iwapo anaweza rejea katika kazi yake ya zamani kama amri za chanjo zitafutwa katika sehemu aliko kuwa akifanya kazi.

"Mazingira ya kazi yamebadilika kwa hali mbaya zaidi, sina uhakika kama bado ningependa kuwa sehemu ya mfumo ambao hauku watendea marafiki wangu nami mema," alisema

Rais wa AMA Prof Robson amesema wafanyakazi wengi wa huduma ya afya ambao waliondoka katika mfumo huo, hawakuwa na uhusiano wowote na amri za chanjo.
We understand that only 0.6 per cent of the healthcare workforce in NSW, for example, left because of a requirement for vaccination
AMA President Steve Robson
"Matatizo makuu zaidi yalikuwa ni shinikizo, uhaba wa msaada kutoka wafanyakazi wa huduma ya afya, mazingira mabaya ya kazi pamoja na mapato mabaya na maswala mengine.

"Tunadhani kuna uwezekano mdogo kuwa kuondoa masharti ya chanjo kutapiga jeki nguvu kazi ya huduma ya afya sana, kwa kweli hili linaweza zua wasiwasi kwa baadhi ya wafanyakazi wa huduma ya afya, kiasi kwamba wanaweza ondoka katika mfumo huo," Prof Robson aliongezea.
Profesa Bennett naye amesema wafanyakazi wanaweza rejea katika mazingira ya kazi ambayo hayana masharti ya chanjo kama mafua iwapo amri ya chanjo ya UVIKO itafutwa.

"Ila kuna weza kuwa hali yakusita kurejea katika kazi za mstari wa mbele kwa sababu hakuna dhamana dhidi ya amri hizo kurejea iwapo aina mpya ya kirusi ita ibuka, nakusababisha hatari kubwa zaidi kwa afya," Prof Bennett alisema.

Prof Collignon ameongezea kuwa kurejea kwa wafanyakazi ndani ya mfumo, kunaweza faidi sehemu ambako kuna uhaba wa wafanyakazi.

SBS imejitolea kutoa taarifa mpya zote za UVIKO-19 kwa jamii zenye lugha la tamaduni tofauti zote nchini Australia. Baki salama na endelea kupata taarifa kwa kutembelea mara kwa mara tovuti ya

Share
Published 23 March 2023 2:23pm
By Sahil Makkar, Yumi Oba
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends