Watu kuminasita wame uawa katika maandamano ya sku mbili nchini Uganda, jeshi la polisi likisema maandamano hayo yame jiri baada yakukamatwa kwa kiongozi wa upinzani maarufu.
Jumatano jeshi la polisi lilimkamata kiongozi huyo maarufu wa upinzani ambaye pia ni nyota wa muziki kwa jina la Bobi Wine, alipokuwa katika kampeni ya uchaguzi mkuu wa 2021 kwa shutma kwamba alivunja sheria za COVID-19, kuhusu mikusanyiko ya umma, na maandamano kuanza punde baadae mjini Kampala.
"Idadi ya vifo imeongezeka kutoka watu 3 hadi watu 16. Bado tuna fanya uchambuzi nakupokea taarifa kuhusu waathiriwa," naibu msemaji wa jeshi la polisi Patrick Onyango alisema.
Katika taarifa aliyochapisha, Bw Onyango alisema kwamba idadi ya majeruhi imefikia watu 65.
Jeshi la Polisi lime walaumu wafuasi wa Bobi Wine kwa machafuko hayo nakusema kuwa, walijibu machafuko hayo kwa gesi zakutoa machoji, risasi za mpira, mizinga ya maji, bakora pamoja na risasi za kawaida kudhibiti maandamano ya vurugu.".

The death toll from protests in Uganda has risen. Source: AFP
Jeshi la Polisi liliongezea kuwa, idadi ya watu 350 walikamatwa.
Joel Ssenyonyi ndiye msemaji wa chama cha Bobi Wine, alieleza shirika la DPA kwamba, Wine alikuwa bado kizuizini Alhamisi na hakuwa ameruhusiwa kumwona mwanasheria wake.
Uganda imeratibiwa kufanya uchaguzi mkuu January, na Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anawania kiti cha urais.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 38, ni maarufu kwa kofia yake nyekundu pamoja na nyimbo zake zakisiasa, na anaufuasi mkubwa miongoni mwa vijana.
Bobi Wine anawania wadhifa wa urais dhidi ya Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30.

People Power supporters are seen in Kampala, Uganda, on 3 November, 2020. Source: AFP
Msanii huyo amekamatwa mara kadhaa, tangu alipotangaza nia zake kisiasa.