Feature

Jinsi yakupiga kura katika uchaguzi wa 2023 wa NSW

Wapiga kura wanao stahiki jimboni NSW, wata elekea katika vituo vyakupiga kura Jumamosi Machi 25, kuwachagua wawakilishi wao wa vikao vya bunge vyavyo. Zoezi lakupiga kura ni lazima kwa kila mtu aliye katika sajili yakupiga kura.

ELECTION22 REID

More than 5.4 million people are eligible to vote in NSW. Source: AAP / DEAN LEWINS/AAPIMAGE

Key Points
  • In NSW, those who are eligible to vote, must enrol and vote in all federal and state elections, as well as local government elections.
  • Aside from English, the NSW Electoral Commission provides information about elections in more than 20 languages.
  • The online voting system iVote will not be utilised this election.
Ikiongozwa na Dominic Perrottet, serikali ya mseto inataka pata ushindi wa nne mfululizo ili ibaki madarakani.

Mpanzani mkuu wa Bw Perrottet kwa wadhifa wa kiongozi wa jimbo lake, ni kiongozi wa chama cha Labor Chris Minns, ambaye atawania uchaguzi kwa mara ya kwanza baada yakuchukua usukani wa chama chake Juni 2021.

Bunge la NSW hutumia mfumo wa nyumba mbili, ambazo ni bunge lakutunga sheria linalojulikana pia kama (nyumba ya chini) na baraza lakutunga sheria linalo julikana pia kama nyumba ya juu.

Uchaguzi wa bunge utawapa fursa wapiga kura katika
fursa yakumchagua atakaye wawakilisha ndani ya bunge lakutunga sheria.

Baraza lakutunga sheria linawanachama 42, na katika kila uchaguzi wanachama 21 huchaguliwa kuhudumu kwa mihula miwili ya bunge, ambayo ni miaka minane.

Kama mazingira yanakuwa magumu kwa mpiga kura kupiga kura yake katika kituo chakupigia kura, anaweza stahiki kuomba kupiga kura kupitia posta.

Maombi yakura kupitia posta, yanastahili pokea na tume ya kura ya NSW, kufikia saa 11 jioni ya Machi 20.

Karatasi za kura zilizo kamilika pamoja na vyeti vya kura ya posta, lazima vipokewe na tume ya uchaguzi ya NSW, kufikia saa kumi na mbili jioni ya Aprili 6.
NSW LABOR POLICE KEY ELECTION ASKS
Chris Minns took on the NSW Labor leadership in June 2021. Source: AAP / BIANCA DE MARCHI/AAPIMAGE
iVote, the online voting system, will not be utilised this election.

Kupiga kura siku ya uchaguzi – Machi 25

Zaidi ya idadi ya vituo 2450 vyakupigia kura vita andaliwa ndani ya makanisa, shule, vituo vya jamii pamoja na katika sehemu zingine kote NSW.

Vituo hivi vitafunguliwa siku ya uchaguzi kuanzia saa mbili asubuhi nakufungwa saa kumi na mbili jioni.

Taarifa kuhusu ambako unaweza pigia kura, inapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya NSW.

Punde unapo ingia ndani yakituo chakupiga kura, wafanyakazi watauliza mpiga kura jina lake, anwani yake, eneo bunge lake na kama wamepiga kura tayari katika uchaguzi huo.

Maelezo hayo yanapo thibitishwa, mpiga kura atapewa karatasi zakupigia kura.

Kama wafanyakazi katika kituo hicho hawawezi mpata mpiga kura kwenye sajili ya kura,
NSW Premier Dominic Perrottet
NSW Premier Dominic Perrottet. Source: AAP / Bianca De Marchi

Nilazima kupiga kura

Jimboni NSW, wapiga kura wanao stahiki na walio sajiliwa, wanatakiwa kupiga kura katika chaguzi zote za shirikisho, jimbo na chaguzi za halmashauri za jiji.

Wanao feli kupiga kura wanaweza pewa adhabu.

Kupiga kura kama hauna makaazi, kama una ulemavu, uko katika jimbo lingine au ng'ambo

Kama watu ambao wamo katika vitengo hivi hawawezi piga kura, hawata pewa faini.

Iwapo wapiga kura wenye ulemavu watahitaji msaada, wanaweza mpeleka rafiki au jamaa wao ambaye anaweza wasaidia kupiga kura yao, au wanaweza omba msaada kutoka wafanyakazi wa uchaguzi.

Kama ni vigumu kupiga kura katika kituo cha kura, wanaweza chagua kupiga kura mapema, kupitia posta, kwa simu au kupiga kura katika kituo kilicho tangazwa.

Kama mpiga kura yuko katika jimbo lingine, wanaweza piga kura katika chakupiga kura mapema au kwa posta.

Wapiga kura ambao wamesajiliwa jimboni NSW ila wakati wa uchaguzi watahitaji kupiga kura kwa posta.

Taarifa katika lugha tofauti

Tume ya uchaguzi ya NSW hutoa taarifa kwa jinsi yakusajiliwa nakupiga kura, nakuhusu wagombea katika lugha

Kutakuwa wafanyakazi na watu wakujitolea wanao zungumza lugha mbali mbali katika vituo vyakupigia kura mapema na katika siku yakupiga kura ambao watakuwa wanavaa baji zinazo onesha lugha ambazo wanaweza tumia kutoa msaada.

Tume hiyo hutoa huduma ya ukalimali kwa simu bure, kwa lugha ambazo hazija jumuishwa kwenye orodha hiyo.

Wafanyakazi wa uchaguzi wanaweza waunganisha wapiga kura na huduma ya ukalimani nakutafsiri yakitaifa (TIS National) kama wanahitaji msaada zaidi katika lugha nyingine katika kituo chakupiga kura.

Ili kupugunza hatari ya taarifa za uongo kuhusu uchaguzi kusambaa ndani ya jamii, Tume ya Uchaguzi ya NSW ime weka sajili yataarifa potovu, itakayo fuatilia naku kosoa taarifa potovu naza uongo kuhusu mchakato wa uchaguzi.

Pata taarifa zaidi kuhusu jinsi yakupiga kura kwenye tovuti hii au pigia simu namba hii 1300 135 736.

Share
Published 3 March 2023 4:10pm
Updated 5 March 2023 6:51pm
By Nikki Alfonso-Gregorio
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends