Kombe la Dunia la FIFA 2022™ lita anza 21 Novemba 2022, na mechi zita peperushwa bure kupitia SBS nchini Australia. Mechi zote 64 zitakuwa mubashara na bure kusikizwa kupitia:
- DAB radio yakigitali
- Mtandaoni
- Kupitia app ya simu ya SBS Radio mobile kwa simu aina za na
Jinsi yakusikiza
Jiunge na vituo vyetu maalum kwa matangazo ya Kombe la Dunia la FIFA 2022™ SBS Football 1, 2 na 3 kwenye redio yako ya DAB, kwenye , au kupitia app ya simu ya SBS Radio bure, kusikiza kila mechi mubashara katika lugha 12.
- SBS Football 1 (inapatikana sasa hivi): inatoa matangazo Mubashara ya Kiingereza ya kila mechi wakati wa michuano, pamoja na miziki ya Kombe la Dunia wakati mwingine wote.
- SBS Football 2 na 3 (itazinduliwa Novemba 14): itatoa matangazo mubashara katika lugha za timu zinazo cheza katika kila mechi.
- SBS Arabic24: matangazo mubashara ya kila mechi katika Kiarabu.
Matangazo ya mechi yanatolewa na washiriki wamatangazo wa Kombe la Dunia™ la FIFA, kutoka sehemu zote za dunia na yatapatikana katika mitandao yote ya SBS katika Kiarabu, Kihispania, Kireno, Kifaransa, Kijerumani, Kiholanzi, Kikroasia, Kipasian na Kiingereza.
Wakati wa mashindano SBS Radio 3 itageuka nakuwa SBS Football 2 - ambapo itatoa matangazo katika lugha ya timu husika katika kila mechi. Kuendelea kusikiza vipindi vya BBC wakati huo wa michuano, tafadhali tembelea kupata matangazo hayo mtandaoni.
Nyimbo za Soka
Kando ya matangazo mubashara ya mechi, jiunge nasi kusikiza miziki yenye mandhari ya soka, nyimbo maarufu kutoka michuano ya zamani zikijumuishwa, pamoja na baadhi ya nyingi bora na mbovu za timu za taifa. Anza uzoefu wako wa Kombe la Dunia mapema na sikiza mubashara SBS Football 1 sasa hivi, kupitia radio ya DAB au kwenye .
Tarehe na wakati wa mechi za Kombe la Duniaᵀᴹ la FIFA
Ratiba ya matangazo katika lugha za timu husika kupitia SBS Radio itatolewa karibu ya mwanzo wa mashindano hayo.
- Hatua yamakundi: Novemba 21 - Disemba 3
- Hatua ya 16: Disemba 4 - 7
- Robo fainali: Disemba 10 - 11
- Nusu fainali: Disemba 14 - 15
- Mechi yakuamua mshindi wa 3 nawa 4: Disemba 18
- Fainali ya Kombe la Dunia: Disemba 19
Washiriki wamatangazo katika lugha za timu zitakazo wania kombe hilo wanajumuisha: BBC, Radio Nacional de España, Radio France Internationale, BAND, beIN, RTP, ARD, SRF, RNE, Radio Oriental Montevideo, HRT, RFI, NHK, NOS, VRT, Polskie Radio, Seoul Broadcasting System.