Utoaji wa chanjo ya Coronavirus nchini Australia katika lugha yako

Serikali ya Australia imetoa ahadi yakuwapa wa Australia wote chanjo za COVID-19 bure. Taarifa hii ina maelezo muhimu unayo stahili jua, kuhusu chanjo kama sehemu ya Mkakati wa Utoaji wa Kitaifa.

Descartan dosis de vacunas COVID-19 por fallas de refrigeración.

Source: Getty Images/Larisa Bozhikova

 hutambua watu wanao pewa kipaumbele na, sehemu kote nchini ambako chanjo zinatolewa. Wafanyakazi wa afya ambao wako katika mstari wa mbele, wafanyakazi wa karantini na mipaka, pamoja na wakaaji katika makazi ya huduma ya wazee na ulemavu, pamoja na wafanyakazi ni miongoni mwa watu ambao wamepewa kipaumbele katika mkakati huo wa utoaji.

Chanjo tatu

Australia itatumia chanjo tatu tofauti ambazo zimetengezwa ng'ambo na, chanjo hizo zote zina hitaji kuchukuliwa mara mbili: chanjo ya , chanjo ya pamoja na chanjo ya .

Watoto wenye chini ya umri wa miaka 16, wata pokea chanjo tu kama ushauri wakimatibabu unadokeza kuwa wana hitaji chanjo hiyo. Hadi wakati huo, hawata pokea chanjo yoyote katika hizo chanjo tatu.

Watu wengi watapokea chanjo hizo katika mahospitali, zahanati zama GP, katika zahanati zakupumua, maduka ya jamii yanayo uza madawa na katika huduma za afya zawa Aboriginal, isipokuwa kwa wale wanao ishi au kufanya kazi katika makazi ya huduma yawazee na, ndani ya vifaa vya huduma yawalemavu ambao watapokea chanjo hizo wanako ishi.
Australia's Coronavirus vaccine roll out
Australia's Coronavirus vaccine roll out Source: Australian Department of Health
Coronavirus vaccine priority population
Coronavirus vaccine priority population (Australia) Source: Australian Department of Health

Mpango wa chanjo kwa jamii zenye Lugha na Tamaduni mbalimbali

Mpango wa utekelezaji wa serikali ya Australia, unalengo la kuwa na upatikanaji na salama kwa watu kutoka mazingira ya tamaduni, kabila na lugha mbalimbali (CALD). 

Wanao toa chanjo lazima washirikiane na mashirika ya jamii na viongozi katika kanda zao, kuhakikisha kuwa zahanati zao zinafanyakazi katika hali ambayo ni salama kitamaduni. Ili hili lifanyike, sehemu ya mpango itahusu kujumuisha wafanyakazi wa CALD katika zahanati zinazo toa chanjo.

Baadhi ya mahitaji yanajumuisha nguvu kazi kutoka mazingira mbali mbali, wafanyakazi wanao zungumza zaidi ya lugha moja na, wakalimani wakutoa taarifa inayo hitajika kuhakikisha watu wanapata dozi ya pili ya chanjo.

Coronavirus vaccine priority population
Coronavirus vaccine priority population (Australia) Source: Australian Department of Health

Chanjo yako ita hifadhiwa katika kumbukumbu ya umma.

 

Lazima serikali ihifadhi baadhi ya taarifa kuhusu watu ambao wanapata chanjo, kwa ajili yakujua nani ambaye ameipokea tayari. Ni jukumu la wanao toa mradi wa chanjo wa Australia, kusajili taarifa ya kila mgonjwa anaye pokea chanjo ya COVID-19.

Taarifa kuhusu hali ya chanjo ya mtu, inatarajiwa kupatikana kupitia mfumo wa My Health Record, Medicare (Taarifa ya Historia ya Chanjo), au cheti itakayo chapishwa wakati wa chanjo, ikifuatwa na cheti ambacho kitatumwa kupitia barua pepe.

 

Kiwango cha chanjo kita tofautiana.  

Inachukua wiki mbili kwa mwili kuanza kutengeza kingamwili, zakujilinda dhidi ya virusi ila, ‘ulinzi’ haumaanishi kuwa na ‘kinga’. Dkt Kylie Quinn ni mtaalam wa kinga katika chuo cha RMIT, ali fafanulia SBS viwango tofauiti vya ufanisi wa chanjo:

Kiwango cha 1 - Zuia maambukizi kabisa
Kiwango cha 2 - kutoweza kuzuia maambukizi ila, inaweza sitisha maambukizi yanayo sababisha ugonjwa.
Kiwango cha 3 - kutoweza kuzuia ugonjwa ila, haiwi ugonjwa mubaya sana

 

Chanjo zote za COVID-19 zina tolewa bure

Chanjo hizo ni bure kwa raia wote wa Australia, wakazi wa kudumu na kila mtu ambaye ana viza. 

Kila mtu nchini Australia ambaye ana viza yamasomo, kazi, ujuzi, familia, uchumba, mkimbizi, muomba hifadhi, viza ya muda ya ulinzi, ubinadam, kanda, mpito au viza maalum, anafuzu kupokea chanjo ya COVID-19 bure.

Watu ambao wako vizuizini, nao pia wanafuzu kupokea chanjo hizo, watu ambao viza zao zimefutwa nao pia wanafuzu kupokea chanjo hiyo.

 

 


Taarifa ya serikali kuhusu Coronavirus



Share
Published 11 June 2021 4:39pm
Updated 12 June 2021 12:42am
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends