Wakazi wa Greater Sydney lazima wavae barakoa katika sehemu zingine za umma za ndani

Wakazi wa Greater Sydney (pamoja na Wollongong, Central Coast na Blue Mountains) sasa wanatakiwa kuvaa barakoa katika sehemu zingine za ndani: maduka makubwa, vituo vya ununuzi, sinema, sehemu za maonyesho, usafiri wa umma, saluni za urembo na watengeneza nywele, sehemu za ibada na maeneo ya michezo.

Father helps daughter with mask -  Getty Images - Morsa

Source: Getty Images - Morsa

Kuanzia Jumatatu, 4 Januari, kwa kukosa kuvaa barakoa hubeba faini ya $ 200. Wakati watoto chini ya umri wa miaka 12 hawajalazimika, inapowezekana, mamlaka za NSW zinahimiza kila mtu avae moja. 

Wafanyakazi wote wa huduma za ukarimu na kasino pia wanahitajika kuvaa barakoa. 

Sehemu za ibada, harusi na mazishi zimewekewa kikomo cha watu 100 na imewekwa sheria ya mtu mmoja kwa kila mita nne za mraba. Klabu za usiku zimepigwa marufuku kabisa. Masomo ya mazoezi yamepunguzwa idadi hadi watu 30 kutoka 50. 

Maonyesho ya nje na maandamano yamepunguzwa hadi watu 500, na kuketi, tiketi, na mikusanyiko ya nje iliyofungwa imewekwa kikomo cha watu 2000. 

Tafadhali angalia miongozo ya mwisho kwa jimbo lako au eneo lako:

 

Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa angalau mita 1.5 kutoka kwa mwingine. Angalia vizuizi vya mamlaka yako juu ya mipaka ya kukusanyika. 

Ikiwa unapata dalili za homa au mafua, kaa nyumbani na upange kupima kwa kumpigia daktari wako au wasiliana na Nambari ya Simu ya Virusi vya Corona kwa Taarifa ya Afya kupitia namba 1800 020 080.

Habari na Taarifa zinapatikana kwenye lugha 63 kupitia 



Share
Published 11 January 2021 8:05pm
By SBS Radio
Source: SBS News


Share this with family and friends