Mazoezi ya mwili na kudumisha lishe bora ni vitu viwili ambavyo unaweza fanya kila siku kudumisha afya nzuri, amesema Profesa wa Mazoezi ya Mwili na Afya Anne Tiedemann.
Mengine yanajumuisha kupunguza kiwango cha matumizi ya pombe, kupunguza uvutaji sigara, pamoja nakuendelea kuwa na uhusiano wakijamii.
1. Mazoezi ya mwili
Prof Tiedemann amesema kuna ushahidi wakutosha kuwa mazoezi ya mwili hukuza situ afya ya mwili, afya ya akili na afya ya jamii ila, husaidia pia kuzuia mwanzo wa magonjwa katika uzeeni.
Chenye mtu atafanya leo au wiki hii, kinaweza kuwa na faida katika siku za usoni, mtaalam kutoka chuo cha Sydney ana fafanua zaidi.
Kuhusu kiwango cha mazoezi ya mwili mtu anastahili shiriki, Prof Tiedemann ana elekeza mtazamo kwa , ambao unatoa mapendekezo kutegemea na umri na kama mtu ana ugonjwa sugu au ulemavu.
“Ujumbe mhimu kuhusu mazoezi ya mwili ni kwamba, ni nzuri kwa kila mtu bila kujali umri au kiwango cha ulemavu tunao.
“Na hata kama hauwezi fikisha kiwango cha mazoezi kinacho pendekezwa katika mwongozo huo, tunajua kupitia utafiti ulio wazi kuwa, kiwango chochote cha mazoezi kina faida nakufanya zaidi kidogo kuliko unavyo fanya kwa sasa, itakuletea faida ya afya."
Ameongezea kuwa mazoezi ya mwili yanaweza kuwa kwa umbo tofauti na silazima yame kupitia michezo iliyo pangwa au mazoezi katika kundi.
“Inaweza kuwa wakati wako wakujiburudisha ukienda kutembea au ukifanya kazi zako nyumbani, kwa hiyo kufanya shughuli nyumbani, kulima shamba, vitu hivyo vyote vinakuza afya.”
2. Dumisha lishe bora
Prof Tiedemann amesema ni mhimu kudumisha lishe bora, kupunguza hatari za muda mrefu za ugonjwa na kupunguza hatari ya unene.
Lishe bora katika chakula chako ni nzuri kwa kupa mwili wako nguvu, kuimarisha mifupa yako nakuhisi una nishati.
“Vitu hivyo vyote ni mhimu sana, kula lishe bora, kuto tumia vyakula vingi ambavyo vime andaliwa viwandani, kuto tumia sukari nyingi ambayo ni swala kubwa katika jamii kwa sasa.”
unataarifa kuhusu aina na kiasi cha chakula, kundi za vyakula na mifumo ya lishe.
Inawahamasisha wa Australia wafurahie aina mbali mbali ya vyakula kutoka kundi tano za vyakula, wakati wanajaribu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye mafuta, vilivyo ongezwa chumvi, sukari na pombe.
3. Punguza matumizi ya pombe na acha kuvuta sigara
“Tunajua hayo ni maswala mhimu sana ya hatari ya hali ya maisha kwa magonjwa mengi,” Prof Tiedemann amesema, kuhusu umuhimu wakupunguza matumizi ya pombe nakuacha kuvuta sigara.
Matumizi ya pombe huchangia katika vifo milioni 3 kila mwaka duniani, pamoja nakatika ulemavu na afya mbaya kwa mamilioni ya watu, kwa mujibu wa shirika la Afya la Dunia.
Data kutoka Australian Institute of Health and Welfare (AIHW), inaonesha kulikuwa vifo 1,452 vilivyo husishwa na pombe katika mwaka wa 2020, asilimia kubwa (73%) vikirekodiwa kwa wanaume.
, uliofanyiwa tathmini 2020, uliweka mwongozo kwa matumizi kupunguza hatari za afya kwa matumizi ya pombe.
Zaidi ya hiyo, Baraza la Saratani linapendekeza , zinajumuisha kuwa na siku ambazo hautumii pombe nakutumia maji unapo hisi kiu.
Sigara inakadiriwa kuuwa takriban .
4. Kuweka uhusiano wakijamii
Prof Tiedemann amesema upweke ni “tatizo kubwa” katika jamii, na hiyo inaweza tokea hatakama mtu anazungukwa na watu wengine, kwa sababu mara nyingi “kuna ukosofu wa uhusiano”.
“Inahusu kuhisi uhusiano na watu wakaribu yako nakuhisi uhusiano na jamii tumoishi.
“Inahusu kuhisi kuwa una umuhimu kwa watu na pia, kuonesha kuwa unawajali wengine. Uhusiano huo wakibinadam ni mhimu sana.”
Amesema uhusiano unaweza patikana katika njia kadhaa, zikijumuisha kujitolea nakujumuika ndani ya jamii.
“[Kujitolea] kunaweza kuwa njia yaku kuza uhusiano kijamii na watu wengine, kuwa sehemu ya kundi nakuwa na kusudi la pamoja, watu wengi hupata michezo kuwa nzuri kwa hilo.
“Una michezo inayo husu timu, nyote mnalengo la matokeo sawia na mna uhusiano hivyo.”
Hata hivyo, ana elezea kuwa baadhi ya watu hufurahia kuwa wenyewe.
“Hatakama [watu hawa] wako wenyewe, bado wana uhusiano huo kupitia hali zingine.”
Shirika la Beyond Blue kwa kutumia teknolojia mbalimbali zinazo jumuisha Skype, Zoom, FaceTime na apps kama House Party huwaruhusu watu kujumuika katika vikundi kupitia mawasiliano ya video.
Shirika hilo linapendekeza pia kuweka ratiba yakujumuika mara kwa mara katika jamii, pamoja nakushiriki katika klabu ya kusoma kitabu, kushiriki katika mashindano ya maswali na majibu, kuchangia chakula cha jioni na familia, kwenda katika sherehe za densi au kushiriki katika mazungumzo jioni na marafiki.
5. Jijulie hali pamoja na wale unao wajali
Vizuizi vyakutoka wakati wa janga la UVIKO-19, vilikuwa mfano mzuri wa sababu yakujijali pamoja na wale unao wajali, Prof Tiedemann amesema.
“Nadhani hiyo ni mhimu sana, najua mimi binafsi kama mfano, ningekuwa na wasiwasikuhusu wazazi ambao ni wazee ambao wamefungiwa kutoka au, kuhakikisha wanakila kitu wanacho hitaji.
“Ila mara nyingi huwa hautambui kuwa una beba dhiki nyingi na wasiwasi. Kwa hiyo, kujijulia hali nakuhakikisha unafanya vitu vizuri kwa ustawi wako binafsi ni mhimu sana.”
Shirika la ambavyo mtu anastahili tumia kila wiki kudumisha afya yao ya akili, hisia zao zikijumuishwa, mwili, usingizi na fikra.
Wasomaji wanao hitaji msaada wanaweza wasiliana na Lifeline kwa msaada wa masaa 24 kwa siku kupitia namba hii 13 11 14, iwapo una hitaji msaada kama umelemewa na fikra zakujiua piga simu kwa namba hii 1300 659 467 na kuna msaada kwa watoto kupitia shirika hili Kids Helpline piga simu kwa namba hii 1800 55 1800 ( msaada hutolewa kwa watoto wenye kati ya miaka 5 na vijana wenye miaka 25). Taarifa ya ziada inaweza patikana hapa na
Shirika la huwasaidia watu kutoka tamaduni na lugha mbali mbali.