Jumanne, Australia iliripoti vifo 43 vya UVIKO-19 vilivyo jumuisha vifo 18 Victoria na vifo 17 New South Wales.
Magharibi Australia imerekodi idadi ya juu zaidi ya kila siku ya kesi mpya za UVIKO-19 (12,390), tangu mwanzo wa janga. Iliripoti pia vifo sita vyakihistoria.
Idadi ya kesi mpya ziliongezeka kote nchini Australia, Victoria ikiripoti idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya kila siku (12,722) na idadi ya watu walio lazwa hospitalini (519) tangu 4 Aprili.
Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, kulazwa hospitalini na vifo kote nchini Australia .
Utawala wa Bidhaa za Matibabu (TGA) inachunguza nakutathmini ripoti za myocarditis (kuvimba kwa moyo) na pericarditis (kuvimba kwa tishu inayo zunguka moyo) katika vikundi vya vijana kutoka chanjo za Pfizer na Moderna.
Imesemwa kuwa myocarditis inajulikana ila madhara ya baadae ambayo "ni nadra". Kawaida ni ya muda mfupi na watu wengi, hupata nafuu baada ya siku chache. Ni kawaida zaidi miongoni mwa wavulana wenye miaka kati ya 12-17 baada ya dozi ya pili.
Kundi la ushauri lakiufundi la Australia kwa chanjo, lina zingatia dozi ya nne (ya majira ya baridi) kwa vikundi vya ziada.
Kwa sasa, dozi ya nne imependekezwa kwa watu wazima wenye miaka 65 na zaidi, wakaazi ndani ya makazi ya huduma ya wazee na walemavu, watu wenye miaka 16 na zaidi ambao wana matatizo sugu ya kinga ya mwili, na watu kutoka jamii yawa Australia wa asili na Torres Strait Islanders wenye miaka 50 na zaidi.
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya