Taarifa mpya kuhusu UVIKO-19: Magharibi Australia yakabiliana na Omicron kwa vipimo vya ziada vya RAT bure na kitengo kipya cha wagonjwa mahtuti

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa Machi 15.

Vifaa vya vipimo vya rapid antigen vyatolewa ndani ya boxi.

Serikali ya Magharibi Australia kwa sasa inatoa vifaa vya vipimo vya RAT 15 bure kwa kila nyumba jimboni humo. Source: AAP Image / Joel Carrett

  • Kuanzia leo, nyumba katika jimbo za Magharibi Australia zinaweza pokea aina ya .
  • Vipimo 10 vya ziada vita tolewa kwa walio jisajili wakati serikali ya jimbo hilo, ilipo toa vipimo 5 vya RAT kwa kila nyumba kwa mara ya kwanza.
  • Amber-Jade Sanderson ni waziri wa afya wa Magharibi Australia, jana alifungua kitengo kipya cha wagonjwa mahtuti chenye vitanda 24 katika hospitali ya  Royal Perth Hospital, ambayo itaanza kuwahudumia wagonjwa kuanzia kesho.
  • Waziri Sanderson alisema "kufunguliwa kwa kifaa hicho ni kwa wakati ukizingatia ongezeko la hivi karibuni, la kesi za UVIKO Magharibi Australia hali ambayo imefikisha uwezo wa kitengo cha wagonjwa mahtuti jimboni humo kuwa vitanda 145".
  • Waziri wa Afya wa Queensland Yvette D’Ath jana alitangaza katika mtandao wa jamii kuwa amepatwa na UVIKO-19.
  • Taarifa hiyo imejiri wakati kamishna wa haki za binadam wa Queensland, Scott McDougall alihoji bungeni ombi la Waziri D'Ath kuongeza muda wa mamlaka ya afisa mkuu wa matibabu hadi Oktoba.
  • Kamati ya utayari ya UVIKO ya Kusini Australia, imekutana asubuhi ya leo kujadili kuregeza vizuizi vya ziada jimboni humo, baadhi ya vizuizi hivyo vinajumuisha kuondoa masharti yakuvaa barakoa, masharti ya kujitenga kwa watu wa karibu ambao wana uviko.

Takwimu za UVIKO-19 Australia

New South Wales imeripoti inawagonjwa 1,032 hospitalini wanao pokea matibabu ya UVIKO-19, kuna wagonjwa 38 pia katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kumekuwa vifo 6 pamoja na kesi mpya 10,689 za UVIKO-19.

Jimboni Victoria, watu 197 wame lazwa hospitalini na watu 24 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti wakati watu 6 wanapumua kwa msaada wa mashine. Jimbo hilo limeripoti vifo 4 pamoja na maambukizi mapya 7,460 ya virusi hivyo.

Tasmania imerekodi kesi mpya 1,376 za maambukizi ya UVIKO-19. Kuna watu 14 ambao wana pokea matibabu ya UVIKO-19 hospitalini, na kuna watu 3 ambao wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.

Na katika ACT watu 40 kwa sasa wamo hospitalini wakitibiwa UVIKO-19, watu 4 kati yao wakihitaji huduma katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kifo kimoja kimeripotiwa na maambukizi mapya 786 ya virusi yame ripotiwa pia.

Nako jimboni Queensland, kumeripotiwa kesi mpya 5,589 za UVIKO-19 pamoja na vifo 10. Watu 246 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na watu 19 kati yao wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.


 


 



 

Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapo chini



Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa chini, kama matokoe ya kipimo chako ni chanya 



Jua  kokote nchini Australia

Kama unahitaji msaada wakifedha, 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika lugha yako kwenye .


Share
Published 15 March 2022 3:17pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends