Taarifa mpya ya UVIKO-19: Victoria yashuhudia ongezeko ya watu wanao lazwa hospitalini wakati NSW imeripoti idadi kubwa ya vifo vya kila siku katika mwezi

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 3 Mei 2022.

The Australian Capital Territory could scrap vaccine mandate for workers in healthcare and education settings next week.

The Australian Capital Territory could scrap vaccine mandate for workers in healthcare and education settings next week. (file) Source: AAP Image/Bianca De Marchi

Jumanne, New South Wales (NSW) iliripoti vifo 23 vya UVIKO-19 takwimu ya vifo ambayo ilikuwa ya juu zaidi tangu 4 Aprili. 

Victoria iliripoti vifo 12 na watu 482 wali lazwa hospitalini. Data inaonesha idadi ya wanao lazwa hosptialini inaongezeka jimboni humo. 

Tazama matukio ya kesi mpya ya UVIKO-19, wanao lazwa hospitalini, na wanao fariki nchini Australia .


Serikali ya The Australian Capital Territory inaweza ondoa amri ya sharti la wafanyakazi kuchanjwa, katika sekta za huduma ya afya na elimu wiki ijayo.

Kusini Australia imegundua kesi yake ya kwanza ya maambukizi ya BA.4 na BA.5 katika wasafiri wakimataifa. BA.4 na BA.5 ni aina ya virusi vya Omicron na vimepatwa tayari NSW na Victoria.  


Dkt Sonya Bennett ni Kaimu Afisa Mkuu wa Matibabu wa Australia, amesema coronavirus na maambukizi ya mafua yanatarajiwa kuongezeka katika msimu wa baridi.

"Kupata chanjo yako ya mafua kabla ya kilele cha msimu wa mafua, kuta kupa kiwango cha juu.

"Kawaida msimu huo huwa kuanzia Juni hadi Septemba katika sehemu nyingi za Australia. Huchukua takriban wiki mbili kwa chanjo kuwa na ufanisi kamili, kwa hiyo kupokea chanjo kabla ya Juni ni bora Dkt Bennett aliongezea.

Naibu Rais wa Marekani Kamala Harris, amepewa ruhusa yakurejea tena kazini katika ikulu ya White House, baada yavipimo vyake vya UVIKO-19 kurejesha matokeo hasi. Alipatwa na UVIKO-19 wiki iliyopita.

 


 




Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, 

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye.  


Share
Published 3 May 2022 2:29pm
Updated 3 May 2022 2:32pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends