- Victoria yaripoti kesi mpya 1,220 ndani ya jamii
- Mamlaka NSW wahamasisha wakaaji kufuata sheria za mikusanyiko kabla ya fainali ya mchezo wa NRL
- ACT yarekodi kesi mpya 38 ndani ya jamii
- Tasmania yarekodi kesi moja ndani ya jamii
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 1,220 za COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo vitatu.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema vizuizi vinahusu kulinda mfumo wa afya nakuheshimu watalaam wa afya. “Kitakacho kuwa uhuru kwetu, kitakuwa ni wakati mgumu kwa mfumo wetu wa afya", alisema.
Jana polisi waliwakamata watu 109, katika maandamano dhidi ya chanjo mjini Melbourne.
Michelle Spence, ni meneja wa waaguzi wa kitengo cha hali mahtuti katika hospitali ya Royal Melbourne amesema tangu Julai, Victoria imekuwa na watu 90 ndani ya kitengo cha hali mahtuti na, hakuna hata mtu mmoja humo aliye kuwa ame pata chanjo kamili.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 667 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo 10, wakati eneo la Greater Sydney lime maliza siku 100 ndani ya amri ya makatazo yakutoka nje.
Waziri wa Afya Brad Hazzard amewahamasisha wakaaji, wafanye tahadhari masaa machache kabla ya fainali ya mchezo wa NRL. "Nyumba yako inaendelea kuwa moja ya sehemu za hatari sana kwa upande wa usambaaji wa virusi," alisema.
Kuanzia Oktoba 11, mtu yeyote jimboni NSW ambaye ni mtu wa karibu wa mtu ambaye amepatwa na COVID-19 na amepata chanjo kamili, ata takiwa kufanya vipimo nakujitenga kwa siku saba badala ya siku 14.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- ACT imerekodi kesi mpya 38 ndani ya jamii, watu 16 kati yao wakiwa ndani ya jamii wakati walikuwa katika hali ambukizi.
- Jimboni Tasmania mvulana mmoja amepatwa na COVID-19, baada yakutua mjini Launceston kutoka Melbourne.
- Queensland haija ripoti kesi yoyote mpya. Fainali ya mchezo wa NRL kati ya Penrith Panthers na South Sydney Rabbitohs, ita endelea jioni ya leo katika kitongoji cha Lang Park.
- Jimbo la Kusini Australia liliripoti kesi mpya mbili mchana wa jana.

Stay home Safe Life - SBS Radio Source: SBS Radio
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: