- Maelfu ya miadi ya chanjo ipo Victoria
- Jimboni NSW, 67.5% yawatu wamepata chanjo kamili
- Zaidi ya 94% ya wakaaji wa Canberra wenye zaidi ya miaka 12 wamepata chanjo moja
- Queensland yarekodi kesi mbili mpya ndani ya jamii
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 1,763 ndani ya jamii, idadi ambay imekuwa kubwa zaidi ya kila siku ya jimbo lolote na wilaya nchini Australia, tangu mwanzo wa janga. Watu wane wame fariki pia.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuna maelfu ya miadi wa chanjo za Pfizer, AstraZeneca na Moderna.
Kuanzia leo, sekta ya ujenzi inafunguliwa ila ni wafanyakazi tu walio chanjwa ndiwo wataruhusiwa kurejea kazini, kama wanafuata miongozo mikali ya usalama ya COVID-19.
Kanda ya Latrobe Valley, itaondoka kutoka makatazo yakubaki ndani kuanzia usiku wa manane usiku wa leo.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 608 ndani ya jamii pamoja na vifo saba.
Idadi ya asilimia 88.5 ya watu wenye miaka 16 na zaidi wamepata dozi moja ya chanjo, wakati asilimia 67.5 wamepata chanjo kamili kufikia saa tano dakika 59 usiku wa Jumapili 3 Oktoba 2021.
Amri zakubaki nyumbani zimengezwa hadi tarehe 11 Oktoba katika miji ya Taree, Forster-Tuncurry na Muswellbrook kwa sababu ya ongezeko ya idadi ya kesi katika maeneo hayo.
Australian Capital Territory
Wilaya hiyo imerekodi kesi mpya 33 ndani ya jamii, 14 kati yazo zilikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii.
Idadi ya asilimia 94 ya watu wenye miaka 12 na zaidi, wamepata dozi yao ya kwanza ya chanjo wakati, zaidi ya asiimia 65 yawatu wame pokea dozi yao ya pili ya chanjo.
Bonyeza hapa
Masaa 24 yaliyo pita nchini Australia
- Australia kufikia kiwango cha 80% ya watu wenye zaidi ya miaka 16 ambao wame pata chanjo kamili, kufikia katikati ya mwezi wa Novemba.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: