- Jimboni Queensland kuanzia saa kumi na mbili jioni ya tarehe 4 Machi, matumizi ya barakao hayatakuwa kuwa lazima katika baadhi ya sehemu. Matumizi ya barakoa yata endelea katika hospitali, makaazi ya huduma ya wazee, makaazi ya walemavu, gerezani, katika viwanja vya ndege na katika usafiri wa umma na ndani ya ndege.
- Kuanzia tarehe hiyo jimboni Queensland, hapatakuwa vikomo kwa idadi ya watu wanao weza jumuika pamoja.
- Kuanzaia Machi, taarifa iliyokuwa ikitolewa kila siku kuhusu UVIKO-19 kwa vyombo vya habari jimboni Queensland itasitishwa.
- Jimboni Victoria kuanzia saa tano dakika hamsini na tisa usiku wa Ijumaa 25 Februari, mapendekezo kwa afya ya umma kuhusu kufanya kazi nakusomea nyumbani, ita ondolewa na amri ya uvaaji wa barakoa utasitishwa katika sehemu kadhaa.
- Matumizi ya barakoa bado yatakuwa lazima jimboni Victoria katika usafiri wa umma, ndani ya texi na gari zakukodi kwa muda, katika ndege, ndani ya viwanja vya ndege, hospitalini na katika vifaa vya malezi.
- Katika shule za Victoria haitakuwa lazima kuvaa barakoa kwa isipokuwa katika shule za sekondari. Wanafunzi kutoka darasa la 3 na wafanyakazi katika vituo vya mafunzo ya mapema pamoja na katika shule za msingi, bado wata takiwa kuvaa barakoa kwa sababu ya viwango vidogo vya chanjo miongoni mwa watoto wenye miaka kati ya 5 na 11.
- Matumizi ya barakoa yata takiwa pia kwa watu wanao fanya kazi katika migahawa ya Victoria na ndani ya duka za bidhaa za reja reja, katika mfumo wa mahakama, haki na katika vituo vya kurekebisha tabia.
- Kuanzia wiki ijayo, hospitali za Victoria zitaweza anza kufanya aina zote za upasuaji tena.
- Waziri wa Afya wa Shirikisho Greg Hunt amesema idadi za kesi za UVIKO-19, zimepungua kwa 90% kutoka kilele cha maambukizi ya Omicron.
- Wanao lazwa hospitalini ni nusu ya idadi ya kabla na, kwa mujibu wa Waziri Hunt, hiyo ni kwa sababu yakupungua zaidi kwa idadi ya visa.
TAKWIMU ZA UVIKO-19 Australia
New South Wales iliripoti ina wagonjwa 1,293, kati yao 71 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kume kuwa vifo 14, na kesi mpya 8,752 za UVIKO-19.
Jimboni Victoria, watu 345 wame lazwa hospitalini, 48 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na 8 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine. Kume ripotiwa vifo 14 pamoja na idadi ya maambukizi mapya 6,786.
Jimboni Queensland, kumeripotiwa kesi mpya 5,583 za maambukizi ya UVIKO-19 pamoja na vifo 5. Watu 394 wame lazwa hospitalini ambako wanapokea matibabu ya UVIKO-19, wagonjwa 34 wana hudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Tasmania haija rekodi vifo vyovyote ila imerekodi kesi mpya 820 za UVIKO-19. Watu 11 wamelazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na watu wawili wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Na katika Wilaya ya ACT watu 41 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na kuna mgonjwa mmoja katika kitengo cha watu mahtuti. Hakuna kifo ambacho kimeripotiwa ila kesi mpya 583 za maambukizi zimeripotiwa.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapo chini
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa chini, kama matokoe ya kipimo chako ni chanya