Taarifa mpya ya COVID-19: Victoria yaongeza muda wa makatazo kwa wiki moja zaidi, na Kusini Australia yatangaza vizuizi vya kiwango cha tano

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 20 Julai 2021.

Wynyard railway station

Commuters wait for buses at Wynyard railway station in the central business district in Sydney, Tuesday, July 20, 2021. Source: AAP Image/Mick Tsikas

  • Makatazo ya Victoria yameongezwa hadi Jumanne 27 Julai 2021.
  • New South Wales imerekodi kifo cha tano kutoka mlipuko wa kirusi cha Delta cha COVID-19.
  • Vizuizi vya kiwango cha 5 vime tangazwa Kusini Australia kuanzia saa kumi n ambili jioni ya leo.
  • Zaidi ya waAustralia milioni 10.1 wamepokea dozi yao ya kwanza, wakati milioni 2.8 wame pokea chanjo kamili.
Victoria
Kiongozi wa jimbo la Victoria Daniel Andrews ametangaza kuwa makatazo ya sasa, yataongezwa hadi saa tano dakika hamsini na tisa za usiku wa Jumanne 27 Julai 2021.

Victoria imerekodi kesi mpya 13 za COVID-19 ndani ya jamii, kesi moja isiyojulikana ikijumuishwa. Kesi tisa kati ya hizo zilikuwa zikijitenga wakati zilikuwa katika hali ya uambukizi. Idadi kamili ya kesi jimboni Victoria ni 96.

Kusafiri kuenda Victoria kwa matumizi ya hadi za eneo nyekundu, kutasimamishwa kwa muda. Matangazo kuhusu msaada wa ziada kwa biashara yanatarajiwa kesho.

Kwa sasa kuna takriban watu wa karibu wa waathirika elfu 15,800, na zaidi ya sehemu za 300 zamaambukizi, zikijumuisha Phillip Island katika eneo la kusini ya jimbo hilo hadi Mildura kaskazini magharibi. 

Pata hapa, katika orodha au ramani.  

New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 78 ndani ya jamii za COVID-19, na kume kuwa idadi ya maambukizi 21 ndani ya jamii. Mwanamke katika miaka ya 50 amefariki katika eneo la kusini magharibi Sydney. Kifo chake nicha 61 jimboni NSW kinacho husishwa na COVID-19 na cha tano katika mlipuko huu wa sasa.

Shirika la Service NSW limefungua maombi ya misaada ya makatazo ya COVID kwa biashara ndogo hadi za kati. Muda wakuwasilisha maombi ya msaada huo utakwisha saa tano hamsini na tisa ya usiku wa 13 Septemba 2021. Kwa taarifa zaidi kuhusu msaada huo, tembelea 

Pata hapa, katika orodha au ramani. Makatazo ya sasa, yata ongezwa hadi saa tano hamsini na tisa za usiku wa Ijumaa 30 Julai 2021.

Katika masaa 24 yaliyo pita, hivi ndivyo hali ilivyo kuwa nchini Australia
  • Jimbo la Kusini Australia limerekodi kesi mpya tano za COVID-19 ndani ya jamii. Kiongozi wa jimbo hilo Steven Marshall,  ametangaza vizuizi vya kiwango cha tano kuanzia saa kumi na mbili usiku wa leo hadi angalau Jumanne 27 Julai. Kwa sasa kuna takriban sehemu 16 za maambukizi. Pata hapa,  katika orodha au ramani.

  • Queensland imerekodi kesi mpya ndani ya jamii, ya coronavirus.

  • Wafanyakazi wote wanane wa meli ya mizigo ambao wana dalili za magonjwa, iliyo tua Fremantle Magharibi Australia, wame patwa na virusi vya COVID-19.
 ni malipo yatakayo tolewa kila wiki kwa watu wanao ishi katika sehemu ambako serikali ya madola imetambua kama sehemu hatari ambako, vizuizi vinavyo dumu kwa zaidi ya siku saba vime sababisha watu hao kupoteza masaa ya kazi au kupoteza mapato. Taarifa inaweza patikana katika  wakati huduma ya simu ya lugha mbali mbali inapatikana kupitia namba hii 131 202.

Sherehe ya Eid al Adha (“Sherehe ya Kafara”) itaisha Ijumaa, 23 Julai. Ni mhimu kujilinda wewe binafsi na wengine wakati wa sala za Eid al-Fitr: 

  • kuchagua kufanyia sala nyumbani 
  • kufuta mikusanyiko mikubwa
  • kuvaa barakoa yako
  • kutumia mkeka wako binafsi wa sala

Hadithi potovu kuhusu COVID-19:

Chanjo ya COVID-19 si salama kwa sababu ili undwa haraka sana.

UKWELI kuhusu COVID-19:

Kila chanjo ya COVID-19 lazima itimize masharti ya usalama, ubora na ufanisi wa Utawala wa bidhaa za matibabu ya Australia almaarufu (TGA). TGA itaendelea kufuatilia kwa karibu chanjo, kutambua haraka nakujibu maswala yoyote yatakayo ibuka kuhusu usalama kati ya Australia na ng'ambo. TGA huchunguza pia ubora wa kila mzigo wa chanjo utakayo tolewa nchini Australia kabla uachiwe.

Nchini Marekani,  umeonesha kuwa karibu kila kifo cha COVID-19 nchini humo, inayo funika aina tofauti za virusi, ziko ndani ya watu ambao hawaja chanjwa.

Mnamo mwezi Juni,  imepata kuwa, kesi 103 kati ya kesi 223 za aina ya virusi vya Delta, vilivyo lazwa hospitalini tangu Februari, walikuwa hawaja chanjwa au walikuwa na dozi moja ya chanjo.


Karantini, Usafiri, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Masharti ya Karantini na vipimo husimamiwa, nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:

ACT  na 
QLD  na 
TAS  na 
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba ruhusa mtandaoni.  kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakutoka Australia. Kuna hatua za muda kwa safari za ng'ambo ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali na, taarifa mpya huwekwa kwenye tovuti ya .





Tembelea huduma ya mawasiliano ya afya ya tamaduni mbali mbali ya NSW:

Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


 
 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila mkoa na jimbo:

 
 
 


Share
Published 20 July 2021 3:08pm
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends